Sherehe zenu Huko Huko Dodoma

Sherehe zenu Huko Huko Dodoma

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Wale vibaraka wa CCM walioshiriki kukubali kupinduliwa maoni ya Wananchi yaliokuwa ndani ya rasimu ya Tume ya Warioba na badala yake kuchomoa na kuchomekea maoni ya mabepari wa CCM ,washerehekee ushindi wao hukohuko Dodoma msije mkarudi nazo mitaani ,sherehekeni hukohuko.Hizo rushwa za laki tatutatu zitawatokea puani ,nazani mlipata ujumbe uliowambia tunawasubiri mitaani ,basi mnasubiriwa kweli.
 
Wengi wa wanawake wengi ni wavurugaji sana ,wakishawishiwa kidogo tu wanajiachia kila kitu
 
Haa haa kwani mtawafanya nini?
Hujui kama intelejensia za ccm zinafanya kazi?
 
Wachakachofanywa watakutana nacho hukohuko mitaani ,hapa yatakuja maelezo ya walichofanywa ,halafu si umeona mitaani kulivyo kaza msuli kwa taarifa yako hakuna popote pale katika nchi hii palipotokea angalau shamra shamra za kuwafurahia miccm kwa kupitisha katiba ,hakuna paliporipotiwa.

Kila palipokuwa na televisheni ya wazi na redio kusikiliza matokeo aliyoyapanga Sita ni watu kuilaani ccm na kumlaani Sita na kundi lakehusikii pongezi ,hiyo ni ishara tosha kuwa mitaani si shwari tena ,kama miccm inavyodhania.
 
Wale vibaraka wa CCM walioshiriki kukubali kupinduliwa maoni ya Wananchi yaliokuwa ndani ya rasimu ya Tume ya Warioba na badala yake kuchomoa na kuchomekea maoni ya mabepari wa CCM ,washerehekee ushindi wao hukohuko Dodoma msije mkarudi nazo mitaani ,sherehekeni hukohuko.Hizo rushwa za laki tatutatu zitawatokea puani ,nazani mlipata ujumbe uliowambia tunawasubiri mitaani ,basi mnasubiriwa kweli.

Kaka Mwiba usiwe makali sana,tunatakiwa tuanze kuelimisha umma kupiga kura ya hapana na pia tujiandikishe wengi iwezekanavyo.Tusiendelee kuwategemea Zanzibar,kwani wao kuna section kwenye katiba yao inayosema kama kukitokea changes zozote ni lazima kura ya referundum ipigwe,napo huko kuna kazi ya ziada.
 
Wananchi wana uelewa mkubwa sana kuliko unavyofikiria wala hawahitaji kufundishwa juu ya kuikataa Katiba ya mapepari ,wameshachoshwa na ahadi za miccm na hii nafasi wanaiona kama ni nyota ya jaha ,lazima wataichezesha kwata miccm kwa kura ya HAPANA ,yaani chance for a life time ,wanaisubiri hiyo kura ya maoni ya kuikataa katiba kama wanaosubiri kukabidhiwa bingo !
 
Mwiba,
Naona pressure ipo juu baada ya Katiba ya CCM kupita. Usiwaaamini watanzania hasa wazanzibari kwani unafiki ndio jadi yetu. Angalia usije kupatwa na shinikizo la moyo katiba ikipita kwa kishindo znz.

Mie mtizamaji tu!!!
 
Na wala hujakosea mkuu....itapita kwa shamrashamra za kufa mtu....watanzania hawa waone tu hivi
 
WaZanzibari wa leo sio wale jana ,Zanzibar kuna muamko nkubwa sana kuna kundi la uamsho hili lina hasira na viongozi wao ,hapo napo ccm walivuruga kuwakamata wale jamaa na kuwaweka ndani na kuwatesa na kuwadhalilisha ,usiniambie watapiga kura ya NDIO wafuasi wao wanahasira si kidogo na karibu asilimia 90 ni wafuasi wa uamsho awe CCM awe CUF au kwengineko hao ni wafuasi wa kidini huna la kuwaambia hao 100% ni HAPANA. Wanafuata Imani na matamko ya viongozi wao ,kiongozi yeyote aliebakia kule Zanzibar basi akisema msiikubali katiba hiyo ujue hatabaki mtu nyumbani wataingia kwenye vituo vya kura kwa DHIKRI !
 
Nakubaliana nawe kuwa Zanzibar ndio tegemeo la mwisho katika kukwamisha huu upuuzi.
 
Nampongeza Sita kwa mafanikio chanya aliyoleta katika siasa za nchi hii. Ameweza kuwaonyesha watanzania kuwa adui wao yu miongoni mwao na asitafutwe nje. Naungana na mzee Warioba kuwa sasa tukutane mitaani ili kujua adui hasa wa watanzania miongoni mwetu ni nani ili kukata mzizi wa fitna.
 
Samaki wamekasirika,
Kuvuliwa wamechoka,
Kusikilizwa wanataka,
Mvuvi ye anacheka,
Waache kupaparika,
Shauri ameshalikata,
Jikoni kwenda pika,
Watulie tuli tegoni,
Mvuvi awatangazieni,
Mvuvi aenda shereheni,
Kelele hataki abadani,
Yatatoka meno bila ganzi,
Waambiwa samaki.
^^
 
WaZanzibari wa leo sio wale jana ,Zanzibar kuna muamko nkubwa sana kuna kundi la uamsho hili lina hasira na viongozi wao ,hapo napo ccm walivuruga kuwakamata wale jamaa na kuwaweka ndani na kuwatesa na kuwadhalilisha ,usiniambie watapiga kura ya NDIO wafuasi wao wanahasira si kidogo na karibu asilimia 90 ni wafuasi wa uamsho awe CCM awe CUF au kwengineko hao ni wafuasi wa kidini huna la kuwaambia hao 100% ni HAPANA. Wanafuata Imani na matamko ya viongozi wao ,kiongozi yeyote aliebakia kule Zanzibar basi akisema msiikubali katiba hiyo ujue hatabaki mtu nyumbani wataingia kwenye vituo vya kura kwa DHIKRI !
Kuhusu Wazanzibar, tunajua jinsi ya kudeal nao. Tumekuwa tukifanya hivyo tangu mapinduzi 1964 na hatutashindwa sasa. Huu ndio ukweli na asiyeutaka let him/her park his bags.
 
Samaki wamekasirika,
Kuvuliwa wamechoka,
Kusikilizwa wanataka,
Mvuvi ye anacheka,
Waache kupaparika,
Shauri ameshalikata,
Jikoni kwenda pika,
Watulie tuli tegoni,
Mvuvi awatangazieni,
Mvuvi aenda shereheni,
Kelele hataki abadani,
Yatatoka meno bila ganzi,
Waambiwa samaki.
^^

Na mimi ngoja nijaribu kutunga la kwangu hapa...!
===============
Samaki sasa ni mshangao
Mahali popote walipo
Mvuvi yu baharini na nyundo
Samaki apate kipondo
Mvuvi hana aibu huyo
Kuvua samaki kwa nyundo
Mvuvi kichwani anamapepo
Bahari usalama wake haupo
Dhoruba la elfu mbili kumi na tano
Laweza kumzoa mvuvi huyo

Samaki wanajiuliza,
mvuvi utani kapitiliza,
kuvua kwa Nyundo si ni miujiza?
Samaki wanaulizana.....!
Wengine wanasemezana
Mvuvi kalewa sifa za kuvua !

..............................
==================
Aisee kumbe inawezekana....haya na wewe endelea.
 
Wanna kimbelembele maccm sijui wanajisifu kwa kuchakachua rasimu ya warioba
 
Back
Top Bottom