Sherehe za kuzaliwa miaka 40 CCM hazitafanyika hadaharani?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Na: Mwanahabari Huru

Tarehe 05/02/2017 Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaadhimisha miaka 40 tangu kuzaliwa kwake. Kwa wakati huo kama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, Mh. John Joseph Pombe Maghufuli ndiye atakuwa mwenyekiti.

Kwa utamaduni wa Chama hiki kikongwe, sherehe zake hufanyikia kwenye uwanja wa wazi ambapo kila mwanachama na mfuasi wa Chama hicho anakuwa na fursa ya kuhudhuria.

Kwa kuwa sherehe hizo ni za kisiasa, na hufanyika kwenye eneo la wazi maana yake ni MKUTANO WA HADHARA.

Je, mwenyekiti wa CCM Taifa kwa wakati huo atalazimika kutengua kauli yake ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa!! ???

Polisi nao je watalazimika kusema kuwa huu ni mwaka 2017 na hivyo ya 2016 yalishapita!! ????

It's just a loud thinking!
 
Yaan unatabiri mbali kote huko. Baada ya kukabidhiwa uenyekit lazma wamtambulishe kwa hadhara,!! Wee subir sasa hv hata sio mbali. Tutaambiwa entelejensia imeona mkutano wa ccm aman tele ila cdm no!!
 
yani polisi wana fanya mambo kitoto sana asee!?sasa eatasema nini tena?duuuh
 
Thubutuu... atoe tamko la kuwa hizo pesa zipelekwe chatyo kutengeneza kiwanda cha madawa..#tz ya viwanda!!
 
Back
Top Bottom