Sherehe za kitaifa

Zlatanmasoud

Member
Dec 19, 2010
71
15
Wakuu ni siku chache tu nyuma ndugu zetu Wa tz bara mlisherehekea Miaka 50 ya Uhuru, Mungu ndie ajuae ni shilingi ngapi ziliteketea katika maadhimisho hayo.

na sasa hivi hapa kwetu visiwani shamra shamra za sherehe za mapinduzi ndio zinashika hatamu, kama kawaida kamati ya sherehe na mapambo inatarajiw kutumia fedha za walipa kodi kufanikisha sherehe hizo.

Swali langu kwa wana JF, jee kuna umuhimu gani wa kufanya sherehe hizi kila mwaka? kwa nn isibaki tu kuwa ni holiday na watu wakabaki tu makwao kutafakari?

Jee ni kwa nn hatusherehekei kila baada ya muda fulani kama baada ya miaka 3 au 5 au 10? Kwann tuwaachie watu wachache wateketeze fedha zetu kwa jina la sherehe ukizingatia bado sisi ni maskini wa kutupwa?
 
mkuu hilo suala ni gumu sana kwa wao kuwaingia akilini ukizingatia kwao ni kama mradi wa kuchota pesa zetu,ipo siku kitaeleweka
 
Uharibifu wa pesa ambazo zingeweza kufanya vitu vingine kama katika sekta za afya, elimu, n.k. Ukizungumzia hili utaitwa mwendawazimu.
 
Back
Top Bottom