KUTOKA FB: SHEIKH SULEIMAN TAKADIR ALIVYOPOTEA KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said July 11, 2017 0
Mohamed Said Salum Ugomvi kati ya
Sheikh Suleiman Takadir na
Mwalimu Nyerere ndani ya ofisi ya TANU pale New Street ni katika matokeo ya historia ya TANU ambayo wana TANU wenyewe walipenda labda yafutike yasijulikane. Nadhani hata
Mwalimu Nyerere hakupenda ugomvi ule uingie katika historia yake. Hakika ni kisa cha kusikitisha. Ugomvi huu alinihadithia marehemu
Mzee Haidar Mwinyimvuababa yake
Sheikh Ahmed Haidar ambae alikuwapo katika mkutano ule 1958 mara tu baada ya TANU kuamua kuingia katika Kura Tatu.
Dr. Tamim ndiye aliyenipeleka kwa
Mzee Haidar nyumbani kwake Magomeni. Alinieleza historia nzima ya
Sheikh Takadir na ya Nyerere katika siku zile za mwanzo hadi
Sheikh Takadir alipofukuzwa TANU. Kisa kizima nimekieleza katika kitabu cha
Abdul Sykes.
Kushoto ni
Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na
Julius Nyerere
Mohamed Said Salum Wakati wa utafiti wa kitabu cha
Abdul Sykes sikuweza kupata picha ya
Sheikh Takadir popote ikawa kama vile huyu mtu hakuwa katika TANU tena kiongozi wa juu kabisa. Picha yake ya kwanza nilikuja kuipata miaka hii ya 2000 na alinipa rafiki yangu marehemu
Abdallah Kihombo nyumbani kwake Ilala. Baadae nikapata nyingine kutoka kwa
Jim Bailey African Archive, Johannesburg...