Shekhe mkuu wa mkoa Kagera, awapigia magoti TANESCO na BUWASA

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
Shekhe mkuu wa mkoa Kagera, Alhaji Haruna Kichwabuta, ameiomba TANESCO na idara ya maji (BUWASA) kutokatisha huduma zao kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

Amebainisha kuwa, amechukua uamuzi huo kuwaomba TANESCO kutokata umeme, kutokana na kufanya ibada usiku katika miskiti mbalimbali, na kusema kuwa shughuli hiyo haiwezi kufanyika gizani.Pia, amewaomba BUWASA, idara ya maji wilayani humo kutokata maji, kwani maji ni muhimu pia katika shughuli zote za kufanya ibada.

Anemelizia kwa kusema kuwa, umeme na maji ni mihimili miwili mikuu na muhimu kuwepo katika kipindi kizima cha mfungo wa Ramadhani, kwa kuwa husaidia sana katika shughuli za ibada zao.
 
Kweli inabidi tuwapigie magoti maana Tanesco pale ambapo unahitaji umeme sana ndipo wanapokutia majanga.
 
Shehe huyu angekua mikioa kama Dar naisi angefanya kitu cha ajabu saaana. Bukoba Umeme unakatika mara moja kwa mwezi Tanesco wanapigiwa magoti?
 
Basi tu ndugu kila habari iliyo mbele yangu naona ni mbaya tu
pole, ndo tuungane katika kutokomezza ubaya huo,,,maana unasababishwa kuwepo,,,basi wewe kama mtu mwingine , ndo usababishe kutokomeza
 
Shehe huyu angekua mikioa kama Dar naisi angefanya kitu cha ajabu saaana. Bukoba Umeme unakatika mara moja kwa mwezi Tanesco wanapigiwa magoti?

nahisi kafanya hivyo kwa msisitizo zaidi,,,,,,,
ndo anataka, hata hiyo mara moja istokee hadi mfungo uishe
 
Masheikh wengine wangejitokeza pia kuomba bei ya sukari ipungue jamani sh 4000? Na mfungo huu tutaisoma namba hadi tuzoee
 
Hivi zamani za Mtume kulikuwaga na umeme?? Na je walikuwa wanafanyagaje hizo ibada zao za usiku?? Na pia je walikuwa wanapigaje Azana??
 
Masheikh wengine wangejitokeza pia kuomba bei ya sukari ipungue jamani sh 4000? Na mfungo huu tutaisoma namba hadi tuzoee

lakini si jana nilimsikia Waziri mkuu kupitia vyombo vya habari mbalimbali kuwa, AMEWAHAKIKISHIA WATANZANIA,,,hususan mwezi wa mfung kuwa SUKARI HAITAZIDI 2,300/= per kilo?
 
lakini si jana nilimsikia Waziri mkuu kupitia vyombo vya habari mbalimbali kuwa, AMEWAHAKIKISHIA WATANZANIA,,,hususan mwezi wa mfung kuwa SUKARI HAITAZIDI 2,300/= per kilo?

nahisi wanaouza 4000 ni majipu
 
Hivi zamani za Mtume kulikuwaga na umeme?? Na je walikuwa wanafanyagaje hizo ibada zao za usiku?? Na pia je walikuwa wanapigaje Azana??

Nimekupenda bure,,,,sina maana hasi.

nimeupenda ubongo wako ulivyochangamka kuhusiana na hili,

Hapa nahisi, Mungu kila siku tunamuomba maendeleo, na kwa sababu ametupatia (kutoka vimuli muli,,,vibatari to umeme), basi tuutumie na ndio maana anasisitiza kutokatwa na maji pia, maana hata vyanzo vya maji kwa sasa, vimeshaingiliwa na vingine kuharibiwa kabisa. hivyo miradi ya maji isibanie.
 
lakini si jana nilimsikia Waziri mkuu kupitia vyombo vya habari mbalimbali kuwa, AMEWAHAKIKISHIA WATANZANIA,,,hususan mwezi wa mfung kuwa SUKARI HAITAZIDI 2,300/= per kilo?
Kwa hiyo waziri mkuu katoa bei elekezi mpya ya sukari ambayo ni 2,300/= badala ya 1,800/=?
 
Back
Top Bottom