Shein akemea Ubakaji Zanzibar.

Shein akemea Ubakaji Zanzibar.

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein jana alikemea vikali vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa Jinsia, alipokuwa akihutubia Baraza la Idd. Baraza hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Salama katika Hoteli ya Bwawani mjini Unguja.

Dkt. Shein alinukuu taarifa ya Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, wanawake na watoto, ambayo inasema kuwa jumla ya watoto wa kike 480 wamebakwa Unguja na Pemba katika kipindi cha tangu Julai 2012 hadi April 2013, wastani wa matukio 48 kwa mwezi, au 12 kwa wiki.

Alifafanua kuwa watoto 53 wameharibiwa katika kipindi hicho na wanawake 273 kudhalilishwa.

Alisema ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba silka, ustaarabu na mila za Kizanzibari zinapotea kwa nguvu huku vitendo vya ubakaji na udhalilishaji vikishamiri.

Dkt. Shein alikumbusha wazazi, walezi, wazee na viongozi mballmbali kutimiza wajibu wao wa kulea pamoja na kusimamia na kuendeleza maadili mema.

Kwa namna ya pekee aliwaomba viongozi wa dini waendelee kukemea maovu na kuamrisha matendo mema, na kuepuka mizozano na migogoro ya kidini. Aliwasihi viongozi hao wa dini wawe mfano wa kuönesha subira na kufuata misingi ya dini kusuluhisha tofauti. Aliwaomba viongozi hao wa dini wasichochee waumini kuvunja amani.
 
Wametoka wapi hao wakaki huko Zanzibar, ambako kuimba nyimbo tu zinazodhaniwa zinamaneno wasiyoyapenda humwagiwa tindikali?
 
Wametoka wapi hao wabaki huko h Zanzibar, ambako kuimba nyimbo tu zinazodhaniwa zinamaneno wasiyoyapenda humwagiwa tindikali?
Huko ndiyo makao makuu ya mafezuri na magaidi wanaojifanya wacha mungu!
 
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein jana alikemea vikali vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa Jinsia, alipokuwa akihutubia Baraza la Idd. Baraza hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Salama katika Hoteli ya Bwawani mjini Unguja.

Dkt. Shein alinukuu taarifa ya Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, wanawake na watoto, ambayo inasema kuwa jumla ya watoto wa kike 480 wamebakwa Unguja na Pemba katika kipindi cha tangu Julai 2012 hadi April 2013, wastani wa matukio 48 kwa mwezi, au 12 kwa wiki.

Alifafanua kuwa watoto 53 wameharibiwa katika kipindi hicho na wanawake 273 kudhalilishwa.

Alisema ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba silka, ustaarabu na mila za Kizanzibari zinapotea kwa nguvu huku vitendo vya ubakaji na udhalilishaji vikishamiri.

Dkt. Shein alikumbusha wazazi, walezi, wazee na viongozi mballmbali kutimiza wajibu wao wa kulea pamoja na kusimamia na kuendeleza maadili mema.

Kwa namna ya pekee aliwaomba viongozi wa dini waendelee kukemea maovu na kuamrisha matendo mema, na kuepuka mizozano na migogoro ya kidini. Aliwasihi viongozi hao wa dini wawe mfano wa kuönesha subira na kufuata misingi ya dini kusuluhisha tofauti. Aliwaomba viongozi hao wa dini wasichochee waumini kuvunja amani.
How many are in jail in relation to those babaric acts? wabakaji hawastahili huruma.
 
I thought Zanzibar ni nchi ya KIISLAMU(dini safi)!!!!

Hao wanaobakwa wanakuwa wamevaaje?...vimini...?...vipedo...!? Au HIJAB!?

Sitegemei mtu kuvaa vazi kama HIJAB alafu akabakwa na hawa Wazanzibar safi waliomwagia Waingereza tindikali!!
 
haaa haaaaa haaaaaaaa
 
Tucheke na kudhihaki hawa wazanzibar kama huku hakuna haya mambo....kwangu mimi ni kulilaani hili jambo kwa nguvu zote, halina dini , kabila wala rangi.
 
Wengi waliamini mambo hayo hayapo Zanzibar kwa sababu ya utamaduni wa Zanzibar unaozingatia sana maadili ya dini.
 
Maalim Seif acharukia dawa za kulevya

Imechapishwa Jumamosi, 05 Januari 2013 00:16
Imeandikwa na Khamis Haji,Pemba

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema njia mwafaka ya kuwaokoa vijana na athari za dawa za kulevya Zanzibar ni kila Shehia kujipanga na kuamua kukataa zisiingizwewala kutumiwa katika eneo lake.
Maalim Seif aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Jumuiya ya Maendeleo ya Watu wa Mtoni (JUWAMPE) katika Shehia ya Madungu, Chake Chake, Pemba.
Amesema athari za uingizwaji na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa Zanzibar na kwamba jamii isipoamka na kuamua kukataa kabisa katika maeneo yao, nguvukazi ya vijana inaweza kupotea.
¡°Tusidhani kwa sababu watoto wetu hawatumii tupo salama, wahusika huwashawishi vijana watumie, hata watoto wa baadhi ya viongozi kama mawaziri, wabunge na wawakilishi ni miongoni mwa walioingia katika matumizi ya dawa za kulevya,¡± alionya Maalim Seif.
Alisema Zanzibar kuna maeneo tayari wakazi wake wameamua kukataa kabisa dawa za kulevya na watumiaji pamoja na wauzaji hawathubutu kuingia katika maeneo hayo.
Aliyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni Shehia ya Mkele na Kwa Ali Nato kisiwani Unguja, ambako awali dawa za kulevya lilikuwa tatizo kubwa, lakini baada ya wakazi wake kuamua kupambana, tatizo hilo limetoweka kabisa katika maeneo yao.
ALISEMA INASIKITISHA KUONA DAWA ZA KULEVYA ZINASAMBAA ZANZIBAR KWA KASI TOFAUTI NA SIKU ZA NYUMA,ambapo zilipatikana na kuuzwa mijini hasa Unguja, lakini sasa zimeenea sehemu nyingi, ikiwa ni pamoja na Pemba na baadhi ya maeneoya vijijini.
Hata hivyo, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha inaendelea kwa kasi kubwa juhudi zake ilizokwishazianzisha kutokomeza dawa za kulevya Zanzibar na ana matumaini makubwa ¡®Zanzibar bila ya Dawa za Kulevya¡¯ itawezekana.
Awali, Maalim Seif alizindua rasmi Tume ya Taifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar, inayohusisha wajumbe kutoka taasisi mbalimbali, zikiwemo za ulinzi na usalama, tume ambayo imeundwa kufuatia Sheria mpya ya kupamba na dawa za kulevya Zanzibar, Nam. 12ya mwaka 2011.
 
Back
Top Bottom