Sheikh Hassan bin Amir, waislam wa Burundi na ukoloni wa Wabelgiji makala kutoka juwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
[5:21 PM, 1/9/2017] +255 687 500 699: Home

Monday, 9 January 2017


r4hxSDJ5A8nu4UkooWsyglzEEIRUc3lt13eQxdohoGS7OAf-O-ilzqm1MjXayL_JFcBxyQpaTmbRaFEqyMDNcCf0izQVhWPifzBvDSFYIJypQ12COaiJHuQXusXaQ9KVo2S7gk7qpxEHrMSMRD28aKgsWRIQunKj94-C-5RIG1lpE584KnHv_cMxIeow1qq2cRlPgP28xGFJIlW_pWEEHibMT_VHissW6jjzobyo-fCqTz9IJnS2FiinZY7x8Z5JfFYDVtvskEQhnxH_2FmF4SHPmUQ9dHOe-YC9hupo14-pHm25P5TqC5-k3rAsX7kJATFcsw8T0EkWwNHuU2mVYegVhDl9MT38a5QsjUn7JsuLoSG76iy5ppt7AhE_25o547R-RO0OXlEFaUG1dRgwrsrKVIZTU0WulFYpZAmz3J81GmelPJ92Gcv0E_Wm8ceGTMCmfShIrB85AxOmCimIgxY35y4uzS7kwvnWqrSaJgrgsFe1rJq0Fe4UovEDWqXFD7HpX4juCRtTdjxg8O0P7ZIxKGRF5IfQFfizjs7V8yTaBF1Gtv3pSUG-Ts8lzMZgx1KJeQuc7GtwiEkD_uYhBzu0xCilGXLKZfWj7-WQW_QVS7b_MkrV=w923-h692-no


535066_204150816599526_54954145838478931_n.png


Waislam wa Burundi katika harakati za kupigania uhuru wa Burundi

Si kwamba Waswahili wa Burundi zama za ukoloni walijibagua na kujitenga mbali na elimu. La hasha! Waswahili walikuwa na elimu ya kutosha zama hizo ukiwalinganisha na makabila mengine. Walikuwa wanatumia herufi za Kiarabu (alphabet arabe) kwa kuandika Kiswahili na walikuwa wanajuwa kupiga hesabu (calcul). Walikuwa na shule zao ambazo ni madrasa. Walikuwa wakiandika tungo mbalimbali ikiwemo mashairi. Walitengwa kwenye elimu kwa maksudi na ukoloni. Hasa ukoloni wa Wabeleji ambao uliwanyima wazi Waswahili elimu mpya ya Kimagharibi na kuwapa Kanisa Katoliki umiliki pekee (monopole) wa kuitoa elimu katika nchi.

Waswahili walilalamika zama hizo wala hawakulala. Waliunda chini ya uongozi wa marehemu Sheikh Amrani Juma taasisi iitwayo ASMARU (Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi) yaani Taasisi ya Kielimu ya Waislam wa Ruanda-Urundi). Na walipeleka malalamiko yao mbele ya Serikali na kuwambia nyiye ni wabaguzi, tunaomba na sisi tupewe ruzuku (subventions) ili tujenge shule zetu na tuwalipe walimu wetu waweze kuwafundisha watoto zetu bila kubadiliwa dini yao ya Uislam na Kanisa ambalo ndio njia lilitumia kubadili imani za watoto baada kuona limeshindwa kuwabadili watu wazima.

Ruzuku hiyo iliombwa kwa sababu pesa hizo ni michango ya raia wanaipa Serikali kwa kulipa kodi mbalimbali, na Waswahili walikuwa ni walipakodi wakubwa. Hata na hivyo Serikali ya kikoloni ilikataa kuwapa chochote Waswahili, lakini la kushangaza ikakubali kuwapa Waprotestanti ambao pia walilalamika. Waprotestanti walipewa ruzuku ya 50,000 F (Franka elfu khamsini) ambazo zilikuwa nyingi sana kwa zama hizo. Hatimaye Waswahili wakapiganisha huku na kule na kupata msaada toka kwa ndugu zao Watanganyika na kujenga shule moja ya watoto wao ambayo ni Jumuiya (Jina la Jumuiyatul Islamiyya fii Tanganyika).

Hiyo shule ipo hadi leo Barabara ya Nane na ya Tisa Buyenzi. Alikuja kutoka Tanganyika Mufti Hassan bin Amir kuzindua shule hiyo. [HASHTAG]#WazeeWetuHawakuwaWazembe[/HASHTAG] Mungu awarehemu !
[5:22 PM, 1/9/2017] +255 687 500 699: Katikati aliyeshika bakora ni Sheikh Hassan bin Amir aliyefikuzwa Tanzania 1968 kwa kutaka kujenga Chuo Kikuu kwa Waislam
[5:23 PM, 1/9/2017] +255 687 500 699: Waislam wa Burundi katika harakati za kupigania uhuru wa Burundi
 
maalim mzee wangu salam kwako
umeongea vyema kuhusu waswahili wa burundi,walikuwa ni watu waliotengwa sana urundi na kuchukuliwa kama wa daraja la chin mno,wengi walibadili majina yao ili kuficha asili yao waonekane si waswahili ili wasibaguliwe,,waliungana na wahutu na watusi wa burundi wapigane wapate uhuru ila mwisho wa siku walikuja kutupwa mbali na kutothaminiwa
 
Back
Top Bottom