Sheikh Abuu Idd: CUF iwe makini na CHADEMA wakati huu wa mgogoro, vinginevyo itazidiwa kete

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

Chama cha Wananchi (CUF) kinapaswa kuongeza umakini katika kadhia ya mgogoro wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba.

Pamoja na ukweli kwamba upo unaoitwa Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa), lakini bado haujakidhi matakwa ya kisheria ya kuwa chombo kamili. Kwa hiyo, kila chama kinachounda huo ‘Ukawa’ kinatakiwa kijue kwamba kinajitegemea chenyewe.

Katika kadhia ya Profesa Lipumba wamesikika baadhi ya viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakimshutumu Profesa Lipumba kwa usaliti na kuridhishwa kwao na mpango wa baadhi ya wanaCUF wasiopendelea kiongozi huyo aendelee kukikalia kiti hicho.

CUF inapaswa isijisahau, iyakumbuke mambo kadhaa. Kwanza, suala la uenyekiti wa Profesa Lipumba uwepo wake au vinginevyo ni mambo ya ndani ya chama hicho ambayo hayaingiliwi na nguvu ya chama kingine.

Pili, kitendo cha CUF ‘kujisahaulisha’ kwamba lengo lake la kushika dola linafanana la Chadema, kinafanya ‘urafiki’ wao kuangaliwa kwa jicho lisilosinzia hata kwa dakika moja.

Tatu, ikumbukwe kwamba Chadema walikumbwa na mgogoro kama huu kwa wao kuondokewa na katibu mkuu wao na walipoanza kumshambulia wala hawakuhitajia msaada kutoka CUF kama ambavyo leo wao wameamua kuisaidia bure CUF.

Nne, siyo vyema kumtazama na kumlinganisha Profesa Lipumba na kiongozi au mwanachama yeyote aliyewahi kufukuzwa ndani ya CUF, kwani kiongozi huyo ni msomi anayethibitishwa na CUF yenyewe na amekaa ndani ya chama hicho kwa muda mrefu takriban miaka 20.

Aidha, kupitia ushawishi wake Profesa Lipumba, chama hicho kimeweza kukubalika Tanzania Bara na ile dhana kwamba CUF ni chama cha watu wa Visiwani ilifutika. Pia, Profesa Lipumba amewekeza ndani ya chama hicho ushauri wa kiuchumi na kisiasa ambao umeitoa CUF huko ilipokuwa na kuifikisha kuwa na hadhi ya juu zaidi.

Vilevile, Profesa Lipumba amegombea mara kadhaa wadhifa wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kujichumia umaarufu mkubwa kisiasa kitaifa na kimataifa.

Hata kushiriki mara kadhaa katika matukio muhimu ya chama hicho ikiwamo maandamano yaliyopelekea yeye kupigwa na kuumizwa mkono, yanaonyesha utayari wake katika kukitumikia chama hicho.

Kwa kuzingatia hayo na mengine zaidi ya hayo, siyo vyema kumthaminisha Profesa Lipumba kwa thamani ya chini inayotosheleza kumhukumu kwa haraka bila ya upembuzi yakinifu. Ni vyema wanaCUF wakaitafakari kwa kina sababu ya Profesa Lipumba kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho kabla ya kuijadili sababu ya ‘kufuta’ kujiuzulu huko.

Ni vyema zaidi wanaCUF wakajiuliza: Je, msaada wa Chadema kwa CUF una mwisho mwema kisiasa? Kama uwepo wa Profesa Lipumba ndani ya CUF ni nafuu kwa Chadema; Je, wangeshabikia aondoke? Hivi timu ya mpira inapoelekeza usajili wa timu pinzani, kuna nini hapo?

Ukweli ni lazima usemwe. Kama upo mpango wa kujisafisha kwa kuambiana ukweli ni vyema basi tuuchambue mchakato mzima uliotumika kumpata mgombea wa kiti cha urais kupitia Ukawa.

Kumjadili na kumhukumu Profesa Lipumba pekee ni kujadili matokeo ya tatizo bila ya kulijadili tatizo lenyewe. Chadema wanafahamu wazi kwamba wao ndiyo chanzo cha kuharibu mpango wa Ukawa katika kumpata mgombea wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka jana.

CUF ilipaswa kulalamika japo kwa kupaza sauti kwa wananchi kwamba utaratibu umevunjwa badala ya kuendelea na mchakato ulioratibiwa na wanaukawa, Chadema walimpokea mgombea ambaye hawana budi ni lazima wampe nafasi ya kugombea kiti cha urais.

Kwa muktadha huo, Profesa Lipumba anapojiuzulu na sababu akaihusisha na mgombea huyo ni lazima Chadema ifanye mbinu ya kuusahaulisha umma wa Watanzania kile kilichotokea na njia fupi ni kuhakikisha Profesa Lipumba hakalii tena kiti chake.

Inashangaza kuona Chadema inamshutumu kiongozi wa chama kingine kwa usaliti badala ya kumshutumu kiongozi wao ambaye kwa nafasi yake ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho aliamua kukihama wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana tena kwa sababu ile ile ya Profesa Lipumba ya kumkataa mgombea ‘mpya’ wa urais aliyepokelewa na Chadema.

Swali la kujiuliza hapo ni: Je, nguvu nyingi za lawama Chadema walipaswa wazielekeze wapi? Je, ni kwa Katibu wao au mwenyekiti wa wenzao? Ni vyema basi tukaanza kutafakari wenyewe na kuongoza njia.

Chadema haimtaki Profesa Lipumba kwa sababu wanafahamu vyema uwezo wake. Hivyo basi atakapodumu tena ndani ya CUF na akagombea tena nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020 tena hata iwe ni CUF peke yao bila ya Ukawa, Chadema watalazimika kutumia nguvu nyingi ili kumkabili Profesa Lipumba.

Kitendo cha Chadema kumnadi mgombea ambaye wao wenyewe ndiyo waliomchafua hapo awali kimewafanya waonekane hawana dhamira ya dhati ya mabadiliko hivyo hawawezi kuaminiwa wala kuaminika na kwa msingi huo wataendelea ‘kukoleza’ moto ili Profesa Lipumba kama hataondolewa ndani ya chama hicho basi anyimwe ushirikiano ili nguvu ya CUF iwe ndogo na Chadema iendelee kubakia kuwa ndiyo chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Pamoja na yote hayo, bado Profesa Lipumba anayo changamoto kubwa mbele ya kuumaliza mgogoro kwani bila ya mazungumzo mafanikio ya CUF hayapo.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa Arrisaalah Islamic Foundation. Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.

Maswali na majibu 0715299749
 
umenena...waliojiweka kando na busara watakutukana lakini CUF halisi watakuelewa.
 
Mijadala huru ndio inatakiwa sasa hapa wenyewe wako wanapewa maelekezo ya kujibu. Ngoja waje utagundua ni wale wale kwa ID zao na hoja zao zinafanana katika kila mijadala.
Hili wanatakiwa kuambiwa kila mara mpaka watakapo kumbuka hawa kwa vichwa vyao.
 
Ila wawe tayari kumpokea msaliti lipumba ,kwann hilo hulisemei ukitaka kusema haki razima uwe mkweli vinginevyo lsbda kama unakwenda ya I......tafakari upya shekhe
 
Unapo zungumza ukweli lazima tukuunge mkono hapo umenena
CUF jihadharini na CHADEMA hawana nia njema na ninyi, kumbukeni ndio hao waliwaiteni ninyi CCM B.
View attachment 420956
Chama cha Wananchi (CUF) kinapaswa kuongeza umakini katika kadhia ya mgogoro wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba.

Pamoja na ukweli kwamba upo unaoitwa Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa), lakini bado haujakidhi matakwa ya kisheria ya kuwa chombo kamili. Kwa hiyo, kila chama kinachounda huo ‘Ukawa’ kinatakiwa kijue kwamba kinajitegemea chenyewe.

Katika kadhia ya Profesa Lipumba wamesikika baadhi ya viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakimshutumu Profesa Lipumba kwa usaliti na kuridhishwa kwao na mpango wa baadhi ya wanaCUF wasiopendelea kiongozi huyo aendelee kukikalia kiti hicho.

CUF inapaswa isijisahau, iyakumbuke mambo kadhaa. Kwanza, suala la uenyekiti wa Profesa Lipumba uwepo wake au vinginevyo ni mambo ya ndani ya chama hicho ambayo hayaingiliwi na nguvu ya chama kingine.

Pili, kitendo cha CUF ‘kujisahaulisha’ kwamba lengo lake la kushika dola linafanana la Chadema, kinafanya ‘urafiki’ wao kuangaliwa kwa jicho lisilosinzia hata kwa dakika moja.

Tatu, ikumbukwe kwamba Chadema walikumbwa na mgogoro kama huu kwa wao kuondokewa na katibu mkuu wao na walipoanza kumshambulia wala hawakuhitajia msaada kutoka CUF kama ambavyo leo wao wameamua kuisaidia bure CUF.

Nne, siyo vyema kumtazama na kumlinganisha Profesa Lipumba na kiongozi au mwanachama yeyote aliyewahi kufukuzwa ndani ya CUF, kwani kiongozi huyo ni msomi anayethibitishwa na CUF yenyewe na amekaa ndani ya chama hicho kwa muda mrefu takriban miaka 20.

Aidha, kupitia ushawishi wake Profesa Lipumba, chama hicho kimeweza kukubalika Tanzania Bara na ile dhana kwamba CUF ni chama cha watu wa Visiwani ilifutika. Pia, Profesa Lipumba amewekeza ndani ya chama hicho ushauri wa kiuchumi na kisiasa ambao umeitoa CUF huko ilipokuwa na kuifikisha kuwa na hadhi ya juu zaidi.

Vilevile, Profesa Lipumba amegombea mara kadhaa wadhifa wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kujichumia umaarufu mkubwa kisiasa kitaifa na kimataifa.

Hata kushiriki mara kadhaa katika matukio muhimu ya chama hicho ikiwamo maandamano yaliyopelekea yeye kupigwa na kuumizwa mkono, yanaonyesha utayari wake katika kukitumikia chama hicho.

Kwa kuzingatia hayo na mengine zaidi ya hayo, siyo vyema kumthaminisha Profesa Lipumba kwa thamani ya chini inayotosheleza kumhukumu kwa haraka bila ya upembuzi yakinifu. Ni vyema wanaCUF wakaitafakari kwa kina sababu ya Profesa Lipumba kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho kabla ya kuijadili sababu ya ‘kufuta’ kujiuzulu huko.

Ni vyema zaidi wanaCUF wakajiuliza: Je, msaada wa Chadema kwa CUF una mwisho mwema kisiasa? Kama uwepo wa Profesa Lipumba ndani ya CUF ni nafuu kwa Chadema; Je, wangeshabikia aondoke? Hivi timu ya mpira inapoelekeza usajili wa timu pinzani, kuna nini hapo?

Ukweli ni lazima usemwe. Kama upo mpango wa kujisafisha kwa kuambiana ukweli ni vyema basi tuuchambue mchakato mzima uliotumika kumpata mgombea wa kiti cha urais kupitia Ukawa.

Kumjadili na kumhukumu Profesa Lipumba pekee ni kujadili matokeo ya tatizo bila ya kulijadili tatizo lenyewe. Chadema wanafahamu wazi kwamba wao ndiyo chanzo cha kuharibu mpango wa Ukawa katika kumpata mgombea wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka jana.

CUF ilipaswa kulalamika japo kwa kupaza sauti kwa wananchi kwamba utaratibu umevunjwa badala ya kuendelea na mchakato ulioratibiwa na wanaukawa, Chadema walimpokea mgombea ambaye hawana budi ni lazima wampe nafasi ya kugombea kiti cha urais.

Kwa muktadha huo, Profesa Lipumba anapojiuzulu na sababu akaihusisha na mgombea huyo ni lazima Chadema ifanye mbinu ya kuusahaulisha umma wa Watanzania kile kilichotokea na njia fupi ni kuhakikisha Profesa Lipumba hakalii tena kiti chake.

Inashangaza kuona Chadema inamshutumu kiongozi wa chama kingine kwa usaliti badala ya kumshutumu kiongozi wao ambaye kwa nafasi yake ya kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho aliamua kukihama wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana tena kwa sababu ile ile ya Profesa Lipumba ya kumkataa mgombea ‘mpya’ wa urais aliyepokelewa na Chadema.

Swali la kujiuliza hapo ni: Je, nguvu nyingi za lawama Chadema walipaswa wazielekeze wapi? Je, ni kwa Katibu wao au mwenyekiti wa wenzao? Ni vyema basi tukaanza kutafakari wenyewe na kuongoza njia.

Chadema haimtaki Profesa Lipumba kwa sababu wanafahamu vyema uwezo wake. Hivyo basi atakapodumu tena ndani ya CUF na akagombea tena nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020 tena hata iwe ni CUF peke yao bila ya Ukawa, Chadema watalazimika kutumia nguvu nyingi ili kumkabili Profesa Lipumba.

Kitendo cha Chadema kumnadi mgombea ambaye wao wenyewe ndiyo waliomchafua hapo awali kimewafanya waonekane hawana dhamira ya dhati ya mabadiliko hivyo hawawezi kuaminiwa wala kuaminika na kwa msingi huo wataendelea ‘kukoleza’ moto ili Profesa Lipumba kama hataondolewa ndani ya chama hicho basi anyimwe ushirikiano ili nguvu ya CUF iwe ndogo na Chadema iendelee kubakia kuwa ndiyo chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Pamoja na yote hayo, bado Profesa Lipumba anayo changamoto kubwa mbele ya kuumaliza mgogoro kwani bila ya mazungumzo mafanikio ya CUF hayapo.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa Arrisaalah Islamic Foundation. Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.

Maswali na majibu 0715299749
 
Kiukweli hizi hoja zimejaa ukweli mchungu. Siasa zetu zimejaa ulaghai ambao msingi wake ni kundi la mtandao ambalo lilivuruga CCM na kujipenyeza upinzani. Sasa Mbowe ana kazi ya kuendelea kuwa na ushawishi ule ule akizungukwa na "ulipo tupo"
 
Back
Top Bottom