Sheikh Abdallah Rashid Sembe shujaa wa kura tatu na azimio la Tabora

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,796
31,808
SHEIKH ABDALLAH RASHID SEMBE: SHUJAA WA KURA TATU NA UAMUZI WA BUSARA WA TABORA

20161224_223739.jpg

Rai Juni 17-23 1999​

KIFO cha Abdallah Rashid Sembe kilitokea Hospitali ya Bombo, Tanga tarehe 22 Mei, 1999. Siku ya pili yake, Jumapili asubuhi kwa wale waliokuwa wanasikiliza Radio One walisikia katika matangazo ya vifo Mwalimu Julius Kambarage akiarifiwa msiba ule. Kisha jina lililofuata likawa la Rais wa Zanzibar Dk. Salmin Amour na baadae mtangazaji akasema habari za msiba ziwafikie ndugu na jamaa wote.

Hili halikuwa tangazo la kifo la kawaida. Si kila siku wananchi wanapata bahati kama hiyo ya kusikia Mwalimu Nyerere akitangaziwa taarifa ya kifo kwenye radio. Ni wazi kuwa wananchi wengi walikuwa wamepigwa na mshangao. Pana uhusiano gani kati ya Sheikh Abdallah Rashid Sembe na Mwalimu Nyerere kiasi ya kifo cha Sheikh aarifiwe.

Wengi hawamfahamu Sheikh Abdallah Rashid Sembe na wengi wataendelea kutomjua hadi hapo Mwalimu Nyerere, wana-historia na CCM yenyewe itakapoamua kuandika upya historia yake na kuwaenzi wale wote waliopigania uhuru wa nchi hii. Hata pale makaburini Msambweni katika makaburi ya Sharif Haidar, CCM walipokuwa wakieleza habari za mchango wa Sheikh Rashid Sembe katika kuasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika habari zilizotolewa zilijaa makosa matupu.

Msomi maarufu na makini, Juma Mwapachu katika taa'zia aliyomwandikia marehemu Dossa Aziz katika gazeti la the african kwa uchungu alisema kuwa, wakati mwingine inakuwa aibu na fedheha unapowasikia viongozi wa CCM wakijaribu kwa shida sana kueleza mchango wasiojua wa mzalendo aliyefariki dunia. Juma Mwapachu akamaliza kwa kumwuliza Mwalimu Nyerere kuwa hadi lini atanyamaza kimya bila ya kuwataja wenzake aliokuwa nao katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hali kadhalika akawauliza wasomi wazalendo kwanini hadi leo hakuna juhudi ya kutafiti na kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Hadi hapo Mwalimu Nyerere atakapofungua kinywa chake kuwaeleza wananchi habari za mashujaa wenzake aliokuwa nao katika harakati za kudai uhuru, wananchi na hasa kizazi cha hivi karibuni kitakuwa kinamtukuza yeye pekee kama shujaa wa uhuru wa Tanganyika. Na wenzake wengi waliomsaidia watabaki hawafahamiki na mwishowe historia nzima ya uhuru wa Tanganyika itatoweka.

Mchango wa Abdallah Rashid Sembe katika kuasisiwa kwa TANU, Tanga 1955

Mwaka 1955 Sheikh Abdallah Rashid Sembe alikuwa na miaka arobaini na mbili akijishughulisha na biashara ya kuuza nazi katika soko la Ngamiani mjini Tanga.

Hali ya siasa katika jimbo la Tanga ilikuwa ni ya kipekee kabisa ukilinganishwa na jinsi hali ilivyokuwa sehemu nyingine za Tanganyika. Ilikuwa ni Tanga tu katika historia ya Tanganyika kuwa dhana mpya ya siasa zaidi ya ule ubwana wa Waingereza, uliongezeka katika uhusiano baina ya Waafrika na watu wa rangi nyingine.

Katika jimbo la Tanga kwa bahati mbaya sana Uarabu ulichukua nafasi ya tabaka la utawala juu ya Waafrika. Dhana hii ilitiwa nguvu na wakoloni ili kuwagawa wananchi na kuwakandamiza Waafrika. Hiki kilikuwa kitu ambacho Waafrika walikuwa hawajapambanacho. Kwa zaidi ya karne moja walikuwa wamezoea ubwana wa Waingereza. Uongozi wa siasa kupitia African Association ulikuwa chini ya watu waliojinasibu kuwa asili yao ni Uarabu zaidi kuliko Uafrika ingawa wengi wao walikuwa na damu ya Kiafrika. Katika hali kama hii African Association Tanga haikuwa na nguvu ya kuwaunganisha wananchi kupambana na ukoloni kama ilivyokuwa sehemu nyingine. Mara chache sana watu waliihusisha ofisi ya TAA Tanga na siasa. Ofisi ya TAA inakumbukwa na kuhusishwa na mahakama ya kadhi ambako Kadhi, Sheikh Ali bin Hemed alihukumu jamii ya Waislamu kwa kutumia sharia.

Mwaka wa 1875 UMCA ilikuwa imehama kutoka Mkunazini Zanzibar kwenda Magila katika Jimbo la Tanga. Ukristo ulianzishwa na kustawi katika nchi ya Wabondei, na vivyo hivyo nafasi za elimu kwa watoto wa Wabondei ambao wengi walibatizwa katika lile wimbi la kuwania nafasi za elimu. Jimbo la Tanga likabarikiwa na kuwa na Waafrika walioelimika sana. Vijana wengi kutoka Ubondei waliingia Makerere College na siasa za kizalendo zilizoanza baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Wabondei walikuwa wamejaa katika utumishi wa serikali ya kikoloni.

Katika hali kama hii ingelitegemewa kuwa hawa wasomi wa Makerere ambao wengi walikuwepo pale Tanga mjini wakifanya kazi wangetoa uongozi katika African Association na kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Hawa Waafrika wasomi kutoka shule za misheni na Makerere badala ya kuwa wapigania haki wakawa watiifu kwa taasisi mbili zenye nguvu, serikali ya kikoloni na Kanisa. Wasomi hawa waliunda vikundi vyao kwa kushawishiwa na Waingereza vilivyokuwa vikijulikana kama Discussion Groups yaani vikundi vya majadiliano. Vikundi hivi vilijitenga na siasa. Kwa ajili hii basi, ilibakia kwa Waislamu "wasiokuwa na elimu" kuunda TANU na kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Hapa ndipo unakutana na Shekh Abdallah Rashid Sembe.

Kikundi cha wafanyabiashara wadogo wadogo katika soko la Ngamiani, Abdallah Rashid Sembe akiwamo kiliitisha mkutano katika ukumbi wa Tangamano Septemba 5, 1955. Waliohudhuria mkutano huo walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Hamis Heri, Peter Mhando, Mohamed Kajembe, Tuwa Abdallah, Dhili Mgunya, Victor Mkello, Mohamed Sadik, Hassan, Peter Ramadhani Jembe na Ali Mohamed. Peter Ramadhani tayari alikuwa mwanachama wa TANU huko Arusha na alikaribishwa mkutanoni ili waasisi wa TANU wanufaike kutokana na uzoefu wake.

Wasomi wa Makerere, uongozi wa TAA na Mwalimu Kihere mmoja wa wanasiasa wa wakati ule hawakuwepo kwenye mkutano huu muhimu. Mkutano ulifunguliwa na Hamis Heri na ulifungwa kwa uamuzi kuwa mkutano mwingine wa kuchagua viongozi wa chama ufanyike tarehe 23 Oktoba. Mkutano uliamua vile vile kuwa juhudi zifanyike kupata wanachama wengi iwezekanavyo. Kiasi kidogo cha fedha kilikusaywa na Harir Omari Siagi alipewa aende makao makuu ya TANU, Dar es Salam kununua kadi sabini za TANU. Abdallah Rashid Sembe alikuwa mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU.

Tarehe 23 Oktoba, wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua viongozi wao wa kwanza. Hamisi Heri alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Peter Mhando Katibu. Jumla ya watu arobaini na tano walihudhuria mkutano huo na wakapewa kadi za TANU. Mwalimu Kihere alihudhuria mkutano lakini hakuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi. Kamati ya wanachama iliundwa kutokana na wale wanachama kumi na moja waasisi waliokutana katika ule mkutano wa kwanza mwezi uliopita.

Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik. Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga. Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU. Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.

Baada ya kufungua tawi la TANU mjini Tanga, uongozi wa chama ulimwalika Julius Mwalimu Nyerere, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Mbutta Milando. Mwalimu Nyerere alifikia nyumbani kwa Hamis Heri. Huu ndiyo ukawa mwanzo wa urafiki kati ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Abdallah Rashid Sembe. Wazee wa Tanga wanakumbuka kuwa wakati wa harakati Mwalimu Nyerere alipata kufanya mikutano mingi ya siri nyumba ya pili kutoka nyumba ya Sheikh Sembe barabara ya kumi na nne Sheikh Sembe akiwa mwenyeji wake. Nyumba hii sasa hivi inamilikiwa na ukoo wa Salim Mbaruku, moja ya koo maarufu mjini Tanga. Baada ya kushindwa kupata nafasi yoyote katika chama, Mwalimu Kihere alipoteza shauku ya siasa. Mwalimu Nyerere alipokuja Tanga kuifanyia kampeni TANU ndipo Mwalimu Kihere alikaribishwa na Mwalimu Nyerere kujiunga na chama. Matokeo ya ziara ya Mwalimu Nyerere Tanga ilikuwa ni kumrudisha tena Mwalimu Kihere katika siasa.

Mabingwa wa kuhamasisha wa TANU enzi zile, Julius Mwalimu Nyerere, Bibi Titi Mohamed walihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja maarufu wa Tangamano. Hii ilikuwa hatua kubwa sana kwa TANU, na kwa harakati dhidi ya ukoloni katika jimbo la Tanga. Haya yalikuwa mapinduzi makubwa kutoka enzi za zile siasa za wasomi katika Discussion Group ambazo kama akina Sembe na wenzake wangeziendekeza uhuru ungelichelewa sana. Baada ya hapo, Mwalimu Kihere alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanga badala ya Hamis Heri, na Amos Kissenge alichaguliwa Katibu. Abdallah Rashid Sembe mmoja wa wanachama wasisi wa mwanzo kabisa wa TANU alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya TANU akiwakilisha Jimbo la Tanga. Sheikh Abdallah Rashid Sembe alidumu katika nafasi hiyo hadi mwaka 1969 akiwa mmoja wa viongozi waliopitisha Azimio la Arusha mwaka wa 1967.
 
mzee wa parojo;wacha watu wale chrismass!
vijarida km hiv unaitwa mwandish nguli
 
Mtanganyika...
Mdomo haumkatai bwana wake...

Sina uwezo wala nguvu wala madaraka ya kukuzuia wewe kustarehe
katika X Mas.

Ikiwa hii historia inakukera huna haja ya kuisoma.
Ukiliona jina la Mohamed Said unapita zako salama wa salmin.

Sidhani kama unahitaji hili kufundishwa na mtu yoyote.

Kwa njia hii utakula X Mas bila bughudha wala kero ya kusoma yale
yanayounguza nafsi yako wala hutakuwa na ugomvi na mtu.

Lakini ukweli utabaki kuwa hiyo si ''porojo,'' bali ni historia ya uhuru wa
Tanganyika iwe unataka au hutaki.

Kuna watu hawazezi kupita makala ya Mohamed Said lazima watasoma
na sababu wanasema ni kuwa wanasoma upya historia ya Tanganyika.
 
xx hiz porojo za hik kizee ndo unachukua km reference
Mtanganyika...
Umehamaki na matokeo yake badala ya kujadili sasa unakuja
na matusi na kejeli.

Kuhusu ''reference'' hakika mimi ni rejea ya historia ya TANU
na uhuru wa Tanganyika waka sisemi hivi kwa kujigamba kwani
huu ndiyo ukweli.

Angalia baadhi ya ushahidi huo hapo chini:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
Mohamed Said: ABDULWAHID SYKES, JAPHET KIRILO, NA EARLE SEATON, 1952
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

Mtanganyika...
Kuna jopo la wasomi linaloongozwa na Prof. Issa Shivji wanaandika
maisha ya Mwalimu Nyerere.

Hapo chini Prof. Shivji na Prof. Saida Othman wananihoji kuhusu
niyajuayo kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere katika kupigania
uhuru wa Tanganyika.

shwjIqdI4FLVktBDl8hMynYKk2oY1OVpiyj0Q6eWuyDOVRGzxrVc-LeDCuPb_pPaWldQOmcKhr1EQc-EumJRyiysX5_ShdRu8LXiM22Do0l7Vn29uTjoajMTnv2bXdBbcUV4eF6AsEAwA61cmqooALPT1kvUsWIDdIuUcyHaNZE7ryQW3S2SQeZH1jd6eqs6lxDyPxz4-MD0Z5qJOhMXXPfhEypB_nbLTTj73aYrvMmq1X8V87H5LdMCN4ioB4DrgvTT-LY54EqejMF96I2mAAf8_j68e5QaK19y87yFImsYITzX5J3-QoYsdm-e090ZmeJLRIqAXatteT7nd0dampeX1DrqBWcRp3g9aFM6RlrfEuWFCVBTA0PSdM4hhd97D2ESFgQ9VfWfxuP6bx_ccHxsE6ovlcX229dAYeieaw1GqNrDBTD_INUHovIeBHxynzpF0nqsegLU1ssxM1pTrYx_2fvnHM6pfdNqFME1r0tJLeky_6YMyeKcATnMF4Dm5lG--5gDoNgnxMRGHJw_wRCREfaiVRwXFWEXledQ9jvvlXJfXKn8kOoTVNRMIWkN6YyaVkoHttys_Avz3CyTJvi4heq_c7c3PjVyO8zRI1vY7Ad1ZNFz=w800-h534-no

Mtanganyika...
Hii picha hapo chini ilipigwa pwani ya Kipumbwi wakati wa utafiti wa kitabu
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' kuhusu historia ya Zanzibar.

Hapo Kipumbwi ndipo walipovushwa askari mamluki kuingia Zanzibar kuja
kushiriki katika kuipindua serikali ya Mohamed Shamte.

Dr. Ghassany ndiyo mwandishi wa kwanza kueleza habari hizi katika kitabu.

bmtgCQLHb_2fj5KABaHMHYKR0PDK6Sh0p651lZQaUMbaoJLu6yL_abUgWlJnhxyynj3T3T-Jngq9YQp59BAAnw_5WNQLOKZxMcKderAAc9ZebA4UDOdTwp7wTs_Ip4MblHIguDbmUIq3Immp3yPYjRSaFdIcBly_ZNc6_NcD5TGtw8tdJ1hKI9Md77Lh0a9MWtBIRC8qLGI8fBngWZk_8lFe16K6VYWKLWRVgVA6a-UhgFPDBKpjyzkMSiOQaYXXIc05VPfA2ZQgX9ClmU1GAOLJrNgJrJw4jJZRrZyda_6_BjIR5LzjXxnzLPII9ouRegjYBoLwqYIX5Ju2JvG80jdXExpCsrcopg10FGBClND8hfXQvluyTU7IF3QWVlQ9NdR3G3XGGQqWZx7PvZ7RYFYyuxNFSlMoPs08rK-klUO2GzwVpoLNqBbDzMK0NafGpg242Si6fLKVag7Eoz-QcLUZi6WaLiFKzEVKp5WrRP8UO0UoZmEIt5Uk03SaIvseYsqev_AaC_Y9mfgTOKrmINktIrfwcQW2rTKjqKhmTToQBjvm2Q87RZDJDD_ePEVX8FJwuTOyxOHcBCo07irQSxEHlXmLpa7c3Rxa0koKUi9tppMZiZqW=w879-h659-no

Mwandishi wa kitabu hiki, Dr. Harith Ghassany alinichukua kama Mtafiti
Msaidizi.

Nina mengi ya kukueleza lakini tusimame hapa kwanza.
 
Sasa hii history mpya ya uhuru wa tanganyika itakuwepo tu Jf !
Nyiokunda,
Historia hii inasomeshwa sasa vyuo vingi duniani.

Binafsi nimetoa mihadhara University of Iowa na University of Northwestern
kuhusu historia hii unayoiita, ''mpya.''

y8yFTxKGQubaEHJimcdehzVXjkSagMsV35XGzaaSCW0k03-JE27WKcX7-UhXvDknImXvVejHs1ozhpMBEBU_5Cki3H_T93Wbc-KIuaxZgzy1CNDB8emH8J4OxhfmhffdfZJVFqHS82PCllZLHoTkBw2R0zyQaftfK4e9aWPrKRJwaqW5nAMoGFPaculdMOyAwlATq-WlmMdPHXp2dlytV5qOdE6i99Razfzh9bDKih5AEgmz00QNl3SzHrQAEYwy3PTcdRjYENwLJrEZso27D41SnfG8I6kEl5v0vn7vJKO7YGtZFCB_ZhVU1pEZtuzkycavyt2VUsgl_0Q99AkAY3mw8XJSuC_B81pjo7OI16e7uBKrQyxz0MXJn0P-8DzCJ1YB624X4WguORiBIc1pm4KZajXzlRNr1lIducs5DFJ9iz3044zn8Nbr2GMpi60_NkkV_Z52F4EJYPTHIAWkSRpTh9f6Cw0z22WN-oqJYu2GHLO5_ZhAecfz30py2kMjdI6H7zccK65KBiW-yUFmyBem_EiQvndKE53BNgMJ7cAhJZJcI66XirzllcUE3IwnaK4MEa3AzpXduPGdHcYuhbctCZ_IP8UUENWrwNNRe_7Rk-jz1Q=w480-h360-no

University of Iowa Department of African History nitafute katika hilo
kundi hapo juu utaniona.

Nimeshiriki katika uandishi wa Dictionary of African Biography (DAB) mradi
wa Oxford University Press na Harvard.

Soma hapo chini kutoka DAB:

DSCN1129.JPG

DSCN1138.JPG

Historia hii haipo JF tu bali iko kwingi duniani.

Hapo chini Prof. James Giblin wa University of Iowa akionyesha nakala ya kitabu cha
Abdul Sykes toleo la kwanza 1998 ofisini kwake.

PwQtwqsM8W-yKdqXUewwFYnYQyF6KYRsoTA4wGz-KQVNGdPeimoOGWrK1HK2NfgwiyQ3bkcSlTaWm94V2jU9h5pp67l4sIAqKrJf6XuDluhdnjgfey_-XZ_V4iYBwaExqxIj2nn0lsJOSX55H-PJVGwKGe2nHLymBqC35SqRzvx5fuPfrSVhQ7MGzddjATEfX5h2vP9QjvhQrvNHhkvrv6K-T3znwFBq1cMTSPDJnAHP-7cOSzdU4WYL26Iw1yzmMmIUCn_ZqDfqJzyJ2d0XYAGBkEPtzggVBwaXyYYN2N_UPoB_2URauIrbytIUfJYXKaNPhdziDnX_Fect4xlMh7QpmBIhALtdhIQNHZ63gvpTOmrYQwpGnw5uibqbgYPiYxqAzMgzO1a2iS7vffaWO6hQOwTjzPtLc52-fqSyOd2UmTbMot57TjnhobtgzsPMorGJDxX0eKAs0OuSVDiRBwr883Rs-X-SBocVAeNf_xquEeqW_KYs2KJB0TDGTRNZAE1JIlLMpCnC-4fUcTPnAUe4ucCjRiZab46bETL_pPVXMQuK9_ERDR6s_Jn1SbQOm-7PaaBMp2Jj9tUrPmQakF99vlicp_Bq11aG_QpSIbUQYkWyFOdXxg=w480-h360-no
 
Fanya juhudi itambulike hapa inchini.
 
Nyiokunda,
Hapana nchini inafahamika sana kwani ndipo ilipoanza katika miaka ya 1980.

Kitabu cha Abdul Sykes kiko toleo la tatu Kiswahili na la pili Kiingereza.
Lakini JF ndiyo waliosaidia sana kufahamika kwa kitabu hiki kupitia mijada
tunayofanya.
 
Mtanganyika...
Umehamaki na matokeo yake badala ya kujadili sasa unakuja
na matusi na kejeli.

Kuhusu ''reference'' hakika mimi ni rejea ya historia ya TANU
na uhuru wa Tanganyika waka sisemi hivi kwa kujigamba kwani
huu ndiyo ukweli.

Angalia baadhi ya ushahidi huo hapo chini:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
Mohamed Said: ABDULWAHID SYKES, JAPHET KIRILO, NA EARLE SEATON, 1952
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

Mtanganyika...
Kuna jopo la wasomi linaloongozwa na Prof. Issa Shivji wanaandika
maisha ya Mwalimu Nyerere.

Hapo chini Prof. Shivji na Prof. Saida Othman wananihoji kuhusu
niyajuayo kuhusu historia ya Mwalimu Nyerere katika kupigania
uhuru wa Tanganyika.

shwjIqdI4FLVktBDl8hMynYKk2oY1OVpiyj0Q6eWuyDOVRGzxrVc-LeDCuPb_pPaWldQOmcKhr1EQc-EumJRyiysX5_ShdRu8LXiM22Do0l7Vn29uTjoajMTnv2bXdBbcUV4eF6AsEAwA61cmqooALPT1kvUsWIDdIuUcyHaNZE7ryQW3S2SQeZH1jd6eqs6lxDyPxz4-MD0Z5qJOhMXXPfhEypB_nbLTTj73aYrvMmq1X8V87H5LdMCN4ioB4DrgvTT-LY54EqejMF96I2mAAf8_j68e5QaK19y87yFImsYITzX5J3-QoYsdm-e090ZmeJLRIqAXatteT7nd0dampeX1DrqBWcRp3g9aFM6RlrfEuWFCVBTA0PSdM4hhd97D2ESFgQ9VfWfxuP6bx_ccHxsE6ovlcX229dAYeieaw1GqNrDBTD_INUHovIeBHxynzpF0nqsegLU1ssxM1pTrYx_2fvnHM6pfdNqFME1r0tJLeky_6YMyeKcATnMF4Dm5lG--5gDoNgnxMRGHJw_wRCREfaiVRwXFWEXledQ9jvvlXJfXKn8kOoTVNRMIWkN6YyaVkoHttys_Avz3CyTJvi4heq_c7c3PjVyO8zRI1vY7Ad1ZNFz=w800-h534-no

Mtanganyika...
Hii picha hapo chini ilipigwa pwani ya Kipumbwi wakati wa utafiti wa kitabu
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' kuhusu historia ya Zanzibar.

Hapo Kipumbwi ndipo walipovushwa askari mamluki kuingia Zanzibar kuja
kushiriki katika kuipindua serikali ya Mohamed Shamte.

Dr. Ghassany ndiyo mwandishi wa kwanza kueleza habari hizi katika kitabu.

bmtgCQLHb_2fj5KABaHMHYKR0PDK6Sh0p651lZQaUMbaoJLu6yL_abUgWlJnhxyynj3T3T-Jngq9YQp59BAAnw_5WNQLOKZxMcKderAAc9ZebA4UDOdTwp7wTs_Ip4MblHIguDbmUIq3Immp3yPYjRSaFdIcBly_ZNc6_NcD5TGtw8tdJ1hKI9Md77Lh0a9MWtBIRC8qLGI8fBngWZk_8lFe16K6VYWKLWRVgVA6a-UhgFPDBKpjyzkMSiOQaYXXIc05VPfA2ZQgX9ClmU1GAOLJrNgJrJw4jJZRrZyda_6_BjIR5LzjXxnzLPII9ouRegjYBoLwqYIX5Ju2JvG80jdXExpCsrcopg10FGBClND8hfXQvluyTU7IF3QWVlQ9NdR3G3XGGQqWZx7PvZ7RYFYyuxNFSlMoPs08rK-klUO2GzwVpoLNqBbDzMK0NafGpg242Si6fLKVag7Eoz-QcLUZi6WaLiFKzEVKp5WrRP8UO0UoZmEIt5Uk03SaIvseYsqev_AaC_Y9mfgTOKrmINktIrfwcQW2rTKjqKhmTToQBjvm2Q87RZDJDD_ePEVX8FJwuTOyxOHcBCo07irQSxEHlXmLpa7c3Rxa0koKUi9tppMZiZqW=w879-h659-no

Mwandishi wa kitabu hiki, Dr. Harith Ghassany alinichukua kama Mtafiti
Msaidizi.

Nina mengi ya kukueleza lakini tusimame napa kwanza.
dr harith kitabu kizima anaeleza maswala ya madrasa;yule nae mwandish! badala aeleze historia ilivyokuwa anaanza kueleza 'chai'

[HASHTAG]#harith[/HASHTAG] + ww ni wazee wa porojo; huyo shivji uliyemuweka hapo ndo msom so ww 'mbabaishaji' aka janja janja!
 
Mtanganyika...
Waweza kusema lolote kuhusu mimi kupelekea kunitukana na kutaka kunifedhehesha.
Uwezo wa kukuzuia sina na unaweza kufanya utakalo kwa mapana na marefu yake.

Prof. Shivji hakika ni msomi wa sifa lakini juu ya kujua kwake hiyo picha
inamuonyesha yuko nyumbani kwangu kanifuata nimweleze historia ya Tanganyika.

Kitabu cha Dr. Harith Ghassany ni kitabu pekee katika historia ya Zanzibar kilichokuja
na mengi mapya yalyofichwa kwa miaka mingi.
 
Mzee MOHAMED SAID mi binafsi naomba niseme kwamba nimeelimika sana kwa kukufuatilia na sijui bila wewe ningefanana na nani katika wasiojua historia ?
Kitabu chako maisha na nyakati za abdul kimekuwa rejea kubwa sana kwangu na kumbe sio mimi tu ni kwa kila asiye na kasumba ya historia ya tz huwa anakitumia

PIGA KAZI MZEE
 
dr harith kitabu kizima anaeleza maswala ya madrasa;yule nae mwandish! badala aeleze historia ilivyokuwa anaanza kueleza 'chai'

[HASHTAG]#harith[/HASHTAG] + ww ni wazee wa porojo; huyo shivji uliyemuweka hapo ndo msom so ww 'mbabaishaji' aka janja janja!
Utafiti unapingwa kwa utafiti nasio porojo mkuu wewe hayo unayoyasema hajaelezea umeyapata kitabu gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom