Huo ndio ukomo wa fikra zao.
Daima siasa na dini havikai chungu kimoja.
Africa watu wengi sana kama huyu Sheikh hawawezi fikra dhahania.
Hawawezi kufanya siasa za kushindanisha falsafa za, kwa mfano, ubepari na ujamaa, kushindanisha vyama, kusema huyu Samia anapingwa si kwa sababu yeye Samia, bali kwa sababu anawakilisha sera za CCM, sera, labda, za kijamaa, au sera zinazojipinga zenyewe hazijijui ni za kijamaa au kibepari, sera zilizopitwa na wakati, na kuna watu wanampinga si kwa sababu yeye ni Samia, bali kwa sababu anawakilisha CCM, anawakilisha sera zilizochoka etc.
Yani watu kama huyu Sheikh lazima waweke personality ya mtu kwenye siasa. Siasa za kukosoa sera hawawezi.
Mtu akija na kusema Samia anaangushwa na sera kwa sababu CCM haina ugatuzi wa madaraka mikoani, hilo suala halihusiani chochote na Samia wala chuki, hilo ni suala la sera za chama na tofauti za kifalsafa.
Sasa Sheikh anaelewa tofauti hizo za kifalsafa kati ya watu wanaotaka ugatuzi wa madaraka mikoani na kwenye serikali za mitaa na wasiotaka?
Sheikh anaelewa nini kuhusu political economy na economy?
Au anabwabwaja maneno ovyo tu?