peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 16,029
- 26,231
Chanzo:Manara Tv
Mchango huo umetolewa katika ibada ya uzinduzi wa jengo la Kanisa Usharika wa Majengo, iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, Dkt. Fredrick Shoo.
Alhaji Shayo, ambaye pia ni mlezi wa Kwaya ya Vijana wa Usharika huo, ametoa pia sare kwa kwaya hiyo pamoja na bima za afya kwa wazee wenye umri mkubwa zaidi kutoka usharikani.
Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Dkt. Shoo amempongeza mfanyabiashara huyo kwa moyo wake wa kujitoa kusaidia jamii bila kujali tofauti za imani au makabila.
“Huyu Ibrahim ni Mwislamu, si Mkristo, lakini ni mmoja wa watu wachache wanaojitolea kwa moyo kusaidia makanisa, misikiti, shule, hospitali na jamii kwa ujumla. Ni mfano wa kuigwa,” amesema Dkt. Shoo.