Shauri la Madai ya wizi wa ruzuku ya CUF kati ya CUF Vs Msajili wa Vyama vya Siasa na CAG

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

SHAURI LA MADAI YA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF KATI YA THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) DHIDI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI (JAJI FRANCIS MUTUNGI) NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:-

LEO Tarehe 20/4/2017 mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera kulikuwa na mashauri matatu yaliyoletwa pamoja yanayohusiana na maudhui tajwa hapo juu.
Miscellaneous Civil Application (Maombi madogo Shauri namba 28/2017) – linahusiana na Amri ya Mahakama kuzuia Lipumba na kundi lake wasipewe fedha za Ruzuku ya CUF.
Civil Application (Maombi Shauri la msingi namba 21/2017) – Linahusiana na CUF kupinga na kuhoji uhalali wa Msajili kutoa kiasi cha fedha za Ruzuku shilingi Milioni 369 kwa Lipumba na kundi lake kinyume na taratibu za fedha na mamlaka halali ya uongozi wa CUF Taifa.
Miscellaneous Civil Application (Maombi madogo shauri namba 34/2017- inahusiana na Profesa Lipumba na Thomas Malima kuomba kuingizwa katika kesi hiyo kwa madai kuwa wana maslahi mapana na shauri hilo.

Maamuzi;

• Mahakama imekubali ombi la Mawakili wasomi Juma Nassor na Hashim Mziray la kuitaka Mahakama Kuu kuongeza muda wa zuio lililotolewa hapo awali (To extend time of Interim Order) la kuzuia fedha za Ruzuku ya CUF kutotolewa kwa Lipumba na wenzake mpaka hapo mashauri hayo yatakapomalizika. Aidha, upande wa Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameweka pingamizi la kuendelea na shauri hili kwa madai kuwa Bodi ya Wadhamini ya CUF iliyofungua shauri hilo siyo halali (invalid Board)
• Kuhusu Ombi la Lipumba na Thomas kuingia katika Shauri hilo Mahakama imepokea maombi hayo na kwa kuwa hawajawasilisha nyaraka hizo kwa CUF na walalamikiwa wengine, Mahakama imeagiza nyaraka hizo ziwafikie wahusika (To be Saved) kabla ya Tarehe 6/6/2017 ili zijibiwe. Hata hivyo, yameonekana makosa ya uandaaji wa Nyaraka hizo zilizoandaliwa na Lipumba na Thomas kwamba wao ni waombaji (Applicants) lakini wamejiorodhesha katika sehemu ya walalamikiwa (Respondents) ambayo ni makosa kisheria.
• Shauri la Msingi namba 21/2017 lililopangwa kusikilizwa Tarehe 24/4/2017 sasa limepangwa kusikilizwa pamoja Tarehe 6/6/2017
• Kutokana na Mashauri yote haya kuwa na muelekeo unaofanana (Similar but not the same cause) Mheshimiwa Jaji Dyansobera ameshauri yakusanywe pamoja (Joint Trial Consolidation) ili yaende sambamba katika kusikilizwa na kutolewa maamuzi yake. Ombi/ushauri ambao utafanyiwa kazi kisheria na Mawakili wetu kuona namna ya kuyaendea masuala hayo baada ya kupokea Nyaraka toka kwa wahusika. Ni kwa msingi huo Mashauri yote yamepangwa kutajwa na au kusilikizwa Tarehe 6 June, 2017 baada ya pande husika kupokea nyaraka husika (Necessary Documents) na kuzijibu ndani ya muda huo.

• Kwa Upande wa Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliwakilishwa na Mawakili wasomi Mhe. Hachi Chang’a na Mhe. Paulina Bendeni na Upande wa waleta maombi mapya (Lipumba) waliwakilishwa na Thomas Malima (Bila Wakili yeyote), ambapo tofauti na wakati mwingine leo kulikuwa na utulivu na kuzingatia Nidhamu ya Mahakama.

Nichukue fursa hii kuwajulisha Wana-CUF na Wapenda mabadiliko wote nchini kuwa Mawakili wetu wanatuwakilisha vyema na masuala yote yako sawasawa na kwamba upangwaji wa Tarehe za Shauri hilo umezingatia taratibu zote za kisheria na majukumu mengine ya Jaji/Mahakama.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

MAHARAGANDE
NMHUMU
maharagande@gmail.com
0715062577/0784001408
 
Naona mshaanza kuicheza ngoma waliyopanga muicheze, Ila mkishtuka 9maybe in 2019) wanataka mcheze (GoT) mziki mnaoucheza sio mnaoupenda mtajua namna ya kufanya.

Kila la kheri
 
Mdogo mdogo hadi Lipumba akose nauli napendekeza next shauri lisikilizwe January 18.
 
Naona mshaanza kuicheza ngoma waliyopanga muicheze, Ila mkishtuka 9maybe in 2019) wanataka mcheze (GoT) mziki mnaoucheza sio mnaoupenda mtajua namna ya kufanya.

Kila la kheri
Na ndio maana mipango ya kumuondoa Buguruni kinguvu wiki ijayo imekamilika .
 
Kitendo cha msajiri kuchota fedha za cuf na kumpatia lipumba ni kinyume na taratibu kwani lipumba alisha ikimbia cuf
 
Naona mshaanza kuicheza ngoma waliyopanga muicheze, Ila mkishtuka 9maybe in 2019) wanataka mcheze (GoT) mziki mnaoucheza sio mnaoupenda mtajua namna ya kufanya.

Kila la kheri

Shida ni Lipumba anataka CCM ishinde majimbo yote yaani sijui atapata faida gani.

Kwa Lipumba sina shida tatizo lipo kwa Magdalene Sakaya,Mbowe na Lowassa walimpigia sana kampeni leo anachofanya ni aibu.
 
Unaweza kusoma sana watu wakafikiri umeelemika kumbe ndio ujinga umezidi anatia sana aibu
 
Kitendo cha msajiri kuchota fedha za cuf na kumpatia lipumba ni kinyume na taratibu kwani lipumba alisha ikimbia cuf
Hatimaye Mutungi kuvunja rekodi ya Africa , kwa kuwa Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa kufungwa jela kwa kosa la wizi wa hela za umma .

Aibu sana !
 
Shida ni Lipumba anataka CCM ishinde majimbo yote yaani sijui atapata faida gani.

Kwa Lipumba sina shida tatizo lipo kwa Magdalene Sakaya,Mbowe na Lowassa walimpigia sana kampeni leo anachofanya ni aibu.
Sakaya ni Mwanamke wa ajabu sijapata kuona ! Tumeingia gharama kubwa sana kumpeleka bungeni .

Unajua watu wa Tabora walikuwa kama " mawe " , sasa kuyabadili na kuwa mikate haikuwa rahisi .
 
Back
Top Bottom