TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA SHARO
MILIONEA HII HAPA Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo
Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi
Tanga akisema leo majira ya saa mbili
usiku kwenye barabara ya Segera Muheza
mtu mmoja alietambulika kwa jina la
Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR
Toyota Harrier akitokea Dar es salaam
kwenda Muheza alipofika eneo la
Maguzonizonga
wilayani Muheza hilo gari lake liliacha
njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa
marehemu umehifadhiwa kwenye
hospitali Teule ya wilaya ya Muheza
Kamanda amesema hakuna kona kali
sana wala ubovu wa barabara kwenye
sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo
gari imehifadhiwa mahali salama kwa
sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe.