Shariff Seif kweli hapa yamemfika ya CUF

Shariff Seif kweli hapa yamemfika ya CUF

flintsky

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
654
Reaction score
747
"" MAALIM SEIF WAAMBIE UKWELI WANA CUF NA WATANZANIA KAMA KWELI UNAMUOGOPA MUNGU

Uliyafanya haya kwa MASLAHI ya nani?

** MAALIM SEIF ni Katibu wa chama Bara naVisiwani. Katibu ndiye mtendaji mkuu. Ni kwa nini uchaguzi uliopita Zanzibar alizindua kampeni za nguvu na kila Jimbo likapewa gari, kila Shehia Pikipiki na kila tawi pikipiki. Awaeleze Watanzania huku Bara kampeni alizindua tarehe ngapi na alizindulia wapi,? ubaguzi mtupu!

** Eti" MAALIM SEIF anashanga PROF IBRAHIM LIPUMBA kuchangiwa PESA ya kampeni na wabunge! Cha AJABU nini? Yeye amekwenda Dodoma Mara kibao kuwabana wabunge wachangie chama na kila uchaguzi hata kama Ni Uchaguzi mdogo wabunge huwa Wanachangia na uchaguzi uliyopita kila mbunge alikatwa asilimia 10 ya kiinua mgongo kwa Ajili ya uchaguzi hilo mbona halisemi?, Na hata utaratibu wa Matumizi ya FEDHA hizo hauhojiwi na mtu yoyote wala hauko wazi.!

** MAALIM SEIF Awaeleze Watanzania alipata wapi mamlaka ya kufanya vikao vya siri 12 yeye na mbowe kule Zanzibar na huku Bara bila Mwenyekiti wake ambaye Ndiye msemaji wa chama kujua wala kuambiwa Vilipokuwa vinakutana, Wala kilichokuwa Kinazungumzwa ?

**MAALIM SEIF Aeleze yeye na Mbowe walipanga kikao Serena Hotel akamtaka PROF. LIPUMBA awepo wapange maswala ya UKAWA kweli PROFESA akawepo. MAALIM SEIF Na Wenzie Wakaanza kumzodoa mbele ya MBOWE, MBATIA, LISSU na BAREGU, Eti PROFESA LIPUMBA awaeleze kikao kwa nini alichukua fomu ndani ya chama ya kugombea URAIS?

**Wote wakaanza kumzodoa kama ameiba yuko peke yake hakuwa na wa kumtetea. Ni maumivu makubwa Yaliyoje! Wakati MAALIM SEIF alilijuwa hili toka ndani ya CUF na yeye ndiye aliyetoa agizo kwa Watendaji wa Ofisi Kuu Kuhakikisha wanalisimamia Jambo hili na Kuhakikisha linakuwa na Ufanisi Mkubwa na kweli likafanyika kwa Ufanisi Mkubwa Watanzania Wakalishuhudia hili LIVE Kupitia ITV Pale UBUNGO PLAZA (Blue pearl ).

Kwa nini MAALIM SEIF aliruhusu hali hiyo ya kudhalilishwa Mwenyekiti wake Mbele yake bila kufanya utetezi wa hali yoyote Wakati akijuwa Jambo hili hata kama ni Makosa limefanywa na Chama ambacho yeye ni Katibu mkuu, Tena akihudhuria hafla hiyo ya Uchukuaji wa Form wa PROF IBRAHIM LIPUMBA !Hivi kuna usaliti unaozidi huu ?

** MAALIM SEIF akiwa Katibu Mkuu alijua fika Baraza Kuu la Uongozi Taifa ( BKUT) liliamua nini kuhusu Prof kuchukua fomu kama Aliona Prof kakosea kile ndio kilikuwa kikao halali cha kumwuuliza, kwanini alikikimbia kama kawaida yake ya kila Chama Cha Wananchi kinapoingia kwenye masuala magumu Bila Sababu za Msingi? Na kwanini aliporejea asikutane na Mwenyekiti wake kujuwa namna ya kuyaendea maamuzi ya Baraza Kuu kama Mtazamo wake haukuendana na maamuzi ya Baraza Kuu?

** Maalim SEIF Atuambie aiwaita kundi la kina MBOWE kule Zanzibar akawaambia CUF haina mpango wowote kuingia kwenye uchaguzi, wala hawana pesa za uchaguzi akawapa siri zote Za chama. Wakati Viongozi wenzake Wanapambana huku na huku Kusaka fedha ya kuingia kwenye uchaguzi yeye anakaa na Viongozi wa kuanika siri za Chake eti hakuna mpango wowote! Alikuwa anafanya hayo ili iweje na kwa MASLAHI ya nani?
Na kwa MAAMUZI ya kikao Gani?

** Maalim alikuwa anatagemea hisani ya Mbowe amsaidie kule Zanzibar atangazwe mwaka 2015 Jambo ambalo hakulijuwa huu ulikuwa ni UTAPELI wa hali ya juu alichokuwa anawaza Mbowe ni maslahi ya CHADEMA kwanza mengine baadae!

**Kudhihirisha hilo baada ya Seif kuporwa ushindi aseme lini CHADEMA au MBOWE walisimama hata kukemea yaliyotokea ZANZIBAR? MBOWE amekuwa mshenga mzuri kwenye hili la PROFESA LIPUMBA kwa misingi ya UKAWA , mbona ya Msingi kama hili kuporwa ushindi hajawaji sema lolote?

** Prof Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Magdalena Sakaya waliona mbele zaidi wakasema kabla ya kuamua nani agombee kwa ticket ya UKAWA ni lazima tuandikishiane ( MOU ) makubaliano ya namna ya kugawana ruzuku na wabunge wa viti maalum vitakavyo patikana kwa chama kinacho simamisha mgombea urais. Maana watapata kura za vyama vyote akaona wanachelewesha akatuzunguka UKUTA na kuanzisha mazungumzo ya UKAWA nje ya UTARATIBU uliowekwa na vyama vinavyounda Umoja huo.

** Leo CHADEMA wana wabunge 48 viti maalum CUF 10, Ruzuku CHADEMA wana Mil 400 wakati CUF ina 130 mil haya yote ni matokeo yaliyotokana na Mura za CUF na kufanywa wasindikizaji kutokana na maamuzi yaliyochochewa na UROHO wa URAIS wa Zanzibar wa Maalim SEIF.
 
Bibi Yule ana matatizo sana
14732137_1798940970395349_8865795482601761278_n.jpg
 
Haya tumeshasikia ila haija halalisha Lipumba kurudishwa ofisini kwa mtutu wa dola na msajili
 
MABOGOJOHA;
Naona picha tofauti ndo wamenitumia huku. Naona wanaume 2 wamesimama karibu tu na hii ni kutokana na kamera ilotumika. Ka kusimama kwao huku kwamfanya mmoja wao kuwa bibi sijui hilo. Labda ni kengeza. Au nisaidia hapo; bibi ni huyu wa kwetu au ni huyo mtasha? Sijawahi kukaa nao hata karibu hivyo sizijui tabia zao ka kuna ubazazi
Aaahhh, mbona rahisi. Nani yuko mbele na nani anailinda mali zake?
 
Back
Top Bottom