Shangaa nikushangae, watushangae malenga

Shangaa nikushangae, watushangae malenga

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,093
Reaction score
34,909
Leo naishika tama, nikijikuna kichwani,
Dunia sasa zahama, imejaa hamkani ,
Sungura kaila nyama, akayawacha majani,
Shangaa nikushangae, watushangae malenga.

Mwiko kukoroga chai, mwenzenu ninauliza,
Na bubu kuwa laghai, hili linanitatiza,
Lagombaniwa papai , uwa halijachomoza,
Shangaa nikushangae, watushangae malenga.

Dagaa linafukizwa, harufu lisijetoa,
Hili nalo lashangaza, pele kuitwa churua,
Na eda hajamaliza , posa keshaipokea ,
Shangaa nikushangae, watushangae malenga.

Ana upara kichwani , kitana cha kazi gani?
Papa kakutwa mtoni, na makaziye ni pwani,
Huyu kavaa miwani , kuficha tongo machoni,
Shangaa nikushangae, watushangae malenga.
 
Jamani kuna Watu wanaweza tuache matan. Mngekuwa mnawatungia wasanii tingefka Mbali up to now. Wasingefliska
 
Back
Top Bottom