Shamsi ateta na Maalim Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamsi ateta na Maalim Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 5, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Written by administrator // 01/11/2011 // Habari-Picha // 16 Comments

  [​IMG] Na Salma Said,
  WAZIRI wa mambo ya ndani Tanzania Shamsi Vuai Nahodha amesema suala la kitambulisho cha kitaifa liko katika mchakato wa kumpata mkandarasi mmoja kati ya wawili waliopatikana.
  Utekelezaji huo utakuwa wa awamu mbili wa kwanza utakuwa kwa wale ambao taarifa zake zinafahamika kama wafanyakazi ambapo utekelezaji wake utaanza Juni mwaka huu na ile ya pili ambao taarifa zao hazifahamiki iliolengwa na wataalam kufanyika 2014.
  Hayo aliyasema wakati akifanya mazungumzo na makamo wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad huko afisini kwake Migombani katika kikao cha kujadili changamoto mbali mbali zinazohusu afisi hiyo ya Muungano.
  Nahodha alishauri kutokana na kuwa suala hilo ni la muda mrefu sasa muda huo ufupishwe na kuwa 2012 alisema kuna umuhimu wa wakandarai hao kutumia maarifa na uwezo wao ili vipatikane vitambulisho vyenye ubora na taarifa nying zaidi.
  Alisema huu ni mradi mkubwa unaohitaji umakini ili kuepuka mahitaji ya kutengeneza vitambulisho vyengine kila baada ya miaka mitano kutokanana na changamoto za kimaendeleo zinazojitokeza.
  Aidha alisema katika utekelezaji wa awamu hii mamlaka mbali mbali zitashirikishwa na Idara ya uhamiji zitahushwa alihakikisha kuwa kila Mzanzibari atastahiki kupata kitambulisho hicho, hivyo kumfanya kuwa na vitambulisho viwili ikiwemo kile cha Mzanzibari.
  Akichangia katika hilo Makamo kwanza wa rais alitaka kufahamu hilo kwa kuzingatia wimbi la uingizaji wa wagei hapa Zanzibar bila ya kuelewa uraia wao hivyo upatikanaji wa kitambulisho hicho utarahisisha kumfahamu mgeni alieingia iwapo ni mtanzania au anatoka nchi nyingine jirani.
  Mapema Waziri Nahodha alisema wizara yake ni moja kati ya zile zinazokabiliwa na changamoto nyingi hivyo kuiomba ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais kumpa kila ushirikiano kusaidia udhibiti dhidi ya wahalifu.
  Alisema bila ya kuwepo mashirikiano kati ya raia na vyombo vya usalama ikiwemo polisi juhudi za kukabiliana
  na uhalifu hazitafanikiwa.
  Aidha alisema wizara yake hivi sasa ina mpango wa muda mfupi wa kuimarisha jeshi la polisi kwa kulipatia vyenzo bora na za kisasa na taluma kwa watendaji wake husuan ile ya sheria na upelezi.
  Imebainika kutokea wimbi la makosa ya wizi wa fedha kupitia mitandao na kuanisha kuwa eneo moja ambalo wizara yake inalenga kulishughulikia mapema zaidi kwa kuamini kuwa kuna umuhimu wa kuwa na mashirikiano na wamiliki na viongozi wa vyombo vya fedha ili kuona jinsi ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
  Akizungumzia suala la madawa ya kulevya Nahoha alisema iwapo serikali itasimamia vyema suala hilo kuna uwezeano mkubwa wakupata mafanikio hususan ya kuwakamata wale wanaoleta badala ya wanaotumia pekee hivyo kuahidi kutoa kila ushirikiano ili kulifanikisha hilo.
  Nae makao wa kwanza wa rais maalim Seif alisema suala la kuanzisha ulinzi shirikishai limeleta mafanikio makubwa ya kuzuiya makosa mbali mbali na kuwatambua wahalifu kwa mashirikiano na polisi.
  Alirudia kauli yake ya juu ya janaga linalolikabili taifa la ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya na kutaka mtirikiano zaidi katika kukabiliana nalo.
  Alisema tatizo lililopo katika sheria la ukosefu wa vituo ya kutolea tiba na taaluma inafanyiwa kazi na ofisi yake ili kuona wale wote wanaopata hatia wanapitiwa katika vituo hivyo baada ya kumaliza vifungo vyao.
  Hata hivyo maalim Seif alisema changamoto kubwa iliopo katika suala hilo ni kukosa uadilifu kwa waatendaji wanaosimamia vita hiyo kwa kigezo kuwa kuna malalamiko kutoka kwa wanchi ya wahalifu kuachiwa mara tu baada ya kukamatwa na kufikishwa vituo vya polisi.
  Aidha alikemea tabia ya akari wa magereza wasio waadilifu ya kuingiza unga huo magerezani kiasi ambacho baadahi ya awafungwa hutoka wakiwa watumiaji wakubwa wa madawa hayo ilhali walipoingia ilikuwa hata harufu haijui.
  Akizungumziam tatizo jengine ambapo alielekeza shutuma zake ni kwa askari wa usalama barabarani kutokana na Tabia yao ya kukamata magari na kukaa pembeni na madereva kwa mazungumzo hali inaashiria kuepo kwa harufu ya rushwa.,hatua aliosema imehangia kuongezeka kwa ajali na vyom bo vibovu.
  Aidha alilaani tabia mbaya ya baadhi ya wafanyakazi wa viwanja vya ndege na bandari vya kuwa omba omba kwa wageni watalii kiasi cha kuwakosesha raha na kuitia aibu nchi .
  Alishauri hatua za haraka zichukuliwe na kuwepo mfumo malum wa kuwatafuta askari waadilifu na kuwapanga katika maaeneo hayo pamoja na kuwabadili kila baada ya kipindi.
  #gallery-1 { margin: auto; }#gallery-1 .gallery-item { float: left; margin-top: 10px; text-align: center; width: 50%; }#gallery-1 img { border: 2px solid rgb(207, 207, 207); }#gallery-1 .gallery-caption { margin-left: 0pt; }
  [​IMG] [​IMG]
  [​IMG] [​IMG]
  [​IMG]
   
Loading...