Shamba la mitiki linauzwa.

Then kwa maelezo haya,thamani ya bilioni 20 kwa wakati huo itakuwa sawa na thamani ya bilioni 5 kwa sasa!!! Means thamani ya hiyo miti kama ni kweli,ni hiyo bilioni tano!

Mkuu kwenye uwekezaji wowote kuna kitu kinaitwa ROI, na ndicho kinachoongelewa hapa and is subject to change as time goes on ie the more the time the higher the rate of return.
So i can proudly conclude that the value i provided is approximately lower than the actual evaluations on the maturity date of the teak trees.. say after 15yrs.
Then compare with the bid price provided above.
 


Kaka utakua una asili ya Ubishi ,
Unaniambia kama siwezi kuzidisha nitafute kikokotozi wakati pale juu umeenda uka-edit baada ya kugundua ulikosea.

Ungekubali tu kua ulikosea ukaweka masifuri matatu zaidi. Hata quote yako niliyoku-copy inakuumbua kua uliandika Trillion 5.

Anyway, hiyo hiyo 5bilion za sasa nayo si haba kwa cost za 45milion. Labda swali liwe kua inawezekanaje shina moja likatoa mbao 50? Hii miti inakua na urefu na upana gani rough estimates??
 
Last edited by a moderator:
Mimi dalali ngoja nitafute mteja pls come again shamba linaukubwa wa ejar ngapi? Pls call me kesho nipate mawasilino yako yangu 0657534233 or email:sokonigbroker@gmail.com
 

Mkuu Shark nakiri makosa hapo na niliedit baada ya kujibu post yako!
Kuhusu uwingi wa mbao uwezekano wa kufika idadi hiyo upo tena mkubwa tu; jiridhishe kwa picha nilizopiga na kuweka kule fb na nitafrahi kama ntapata msaada wa kuzitundika kwenye uzi huu maana simu yangu haina uwezo!
Angalizo zuri ni hivi kwenye uvunaji wa miti hii hakitupwi kitu labda vijitawi vidoogo vya mwisho mwisho size ya fimbo! jiulize kwann? ni uthamani wake hii miti! natamani aje mtu anaedeal na export ya magogo ya mitiki aweke clarification
 
Last edited by a moderator:
Mimi dalali ngoja nitafute mteja pls come again shamba linaukubwa wa ejar ngapi? Pls call me kesho nipate mawasilino yako yangu 0657534233 or email:sokonigbroker@gmail.com

Mkuu dalali A.Abdon kila kitu nimeweka hapa kwenye uzi. Itakuwa heri kama utaleta mteja ila tahadhari tamaa ya pesa mingi na ile janjajanja ya kidalali tutamuumiza mwenye mali. Anyway ni asbh tayari, tutaftane tujue jinsi ya kufanikisha mchakato huu bila athari yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu siku hizi elimu iko kiganjani mwako, jaribu ku google uone uthamani wa mitiki. Kwa haraka tu ni kwamba miti hii ni very durable hutumika kutengenezea low surfaces boards za ndege na meri. Na matumizi mengine kedekede!

....mkuu tuwekee link tuone hiyo thamani
 
....mkuu tuwekee link tuone hiyo thamani

Mkuu kwani mpaka link? kwanini usiniamini mimi wakati hata hiyo link itakuwa imeandikwa na mtu mwenye experience kama mimi? tena ni bora ukaniamini mimi kwani unaweza kuuliza swali na nikakujibu papo kwa papo.
Fuatilia posts zote za uzi wangu naamini utakubaliana na mimi kisha njoo ununue shamba.
 

Nisamehe kwa uvivu wangu, nina ugonjwa niko inquisitive sana. Katika biashara angalia scenario zote unapowekeza, naona wewe umekokotoa faida tu, bila kuweka gharama, bila kuweka hasara zinazoweza kutokea.
Kuna mashamba mengi sana ya mitiki ambayo itaanza kuvunwa kuanzia miaka saba ijayo, nadhani unaelewa bidhaa ikiongezeka sokoni bei inashuka. Magogo ya Bubenga ni magogo ghali sana Marekani na Ulaya, lakini ukipanda basi mwendo wa masaa kama 50 tu kwenda Congo hapo yanapotoka bei yake utacheka! Kwenye hizi biashara mara nyingi anayefaidika mara nyingi ni mtu wa kati. Sisemi kwamba hiyo miti haina faida, ina faida sana. Hilo shamba la ekari tano mtu akiwekeza say 30M hata ukipata around 800M ni faida kubwa ndani ya miaka kumi kama una pesa ya kuweka. BTW, kwa nini usimsaidie huyo mzee mshauri aende benki kuchukua mkopo? kama shamba lina hati zote kwa hakika atapata mkopo kama atawasilisha business proposal yenye ushawishi. MSIWE WAVIVU WA KUWASAIDIA WAZEE, NI UBINAFSI KUANGALIA TU CHA JUU UTAYOPATA KAMA AKIUZA SHAMBA WAKATI UNGEWEZA KUMSAIDIA MAWAZO BORA ZAIDI.
 
Mkuu CYBERTEQ nashukuru kwa kuiona kweli ndani ya hesabu ulizohitaji.
Sahau kuhusu kushuka kwa thamani ya mitiki sema soko linachafuliwa na wale wanaoexport magogo ambayo hayajakomaa vilivyo kushindwa kupambana na soko.
Leo hii mbao za mninga zimekua adimu lakini pamoja na yote ubora, thamani na demand yake isingeshuka hata kama ingezagaa sokoni.
Kuhusu kumshauri mzee juu ya mkopo nimeimba sana ila hataki na umri wake hawezi kufanya biashara tena. Nilimuona anipe document niprocess mkopo, nikifanikiwa nimpe hela au awe mmoja wa shareholder wa kampuni yetu still amekataa mchakato huo.
Sina tamaa ya hela mimi na kuweka kwangu tangazo humu ni katika hali ya kumsaidia. Angalia bandiko langu ni la lini na nilipotezea ila mzee ameendelea kunisisitiza..
 
Last edited by a moderator:
Habari! Naomba niulize..

Zina miti ngapi kwa sasa hivi zimesha pandwa ambazo zina umri wa miaka saba?
 
Habari! Naomba niulize..

Zina miti ngapi kwa sasa hivi zimesha pandwa ambazo zina umri wa miaka saba?

Salama mkuu!
Nachelea kutoa hesabu zitakazoleta ukinzani kiuhalisia, maana sijahesabu na sikupanda mimi hiyo mitiki kiasi cha kujiridhisha idadi yake. Kama umesoma vizuri bandiko langu bila shaka utakuwa umejionea mwenyewe ukubwa wa miti.
Nikushauri kitu, tenga muda wako vzr upitie kila post ktk bandiko langu. Utaona uthamani wa mitiki na bila shaka utachukua hatua maridhawa juu ya kununua shamba hili.
Unanunua kwa 45M unenda kuprocess mkopo wa 150M.
Huu ndio ukweli wenyewe na laiti kama angejitojeza mtu anikope 45M ningenunu shamba, nikaprocess mkopo aftr three weeks nakupa 47M. Fursa haitatokea tena hii.
 
Wakuu shamba bado lipo. Changamkeni!
 
Salama wakuu!
Nimerudi tena kwa awamu nyingine kwa sura tofauti kabisa katika kujinufaisha na fursa zilizopo katika uwekezaji wa kupanda miti.
Nipo hapa kuwatafta wajasiriamali waliopiga hatua kiabiashara kiasi cha kuwa na annual sales turnover ya atleast Tshs Milioni 100.
Nia hasa ni kupata wasaa wa kuchukua mkopo kwa kutumia hili shamba kama collateral na kuona namna ya kurejesha huu mkopo kwa utaratibu maalum tutakaofikia.
Nawakaribisheni sana wadau.
 
Kisima jaribu kulitangaza shamba hilo kwa kutumia vyanzo vingine.
 

Wewe ni dalali??
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…