Mondoros
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 629
- 474
Mimi si mwandishi mzuri na sina utaalam katika kuandika vema mbele ya waandishi mahiri na magalacha wa habari wanaoandika na maandiko yao na kusomeka na watu wengi yakabaki akili mwa watu kwa miaka na miaka.
Hata hivyo nawaomba radhi.L nanataka nijaribu kuandika kitu ninachokipa kichwa cha maneno "Ujasiri wa Shaka ni adui wa Shaka".Kwanini ni jasiri na ujasiri alionao sasa umegeuka na kuwa ni uadui huku akisakamwa kwa mizengwe na baadhi ya wanasaiasa wenye pupa ya madaraka na vyeo.
Kwanza nijuavyo Shaka wakati akiingia umoja wa vijana pale Makao makuu Dar es Salam na kuwa kama Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Mbunge Sixtus Mapunda, nathubutu kutamka jumuiya iliikuta ikiwa ICU. Ilikuwa ikiendeshwa kimzabwamzabwa, shaghalabaghala au kwa lugha nyingine nyepesi mambo yalikuwa yakienda ndivyo sivyo.
Haikuwa na haiba au muonekano kama ilivyo sasa chini ya utendaji wa Shaka . UVCCM imepata heshima na amana yake mbele ya jamii na kurudisha hadhi yake kama ilivyokuwa enzi za TANU /ASP Youth League, baadae UVCVM katika miaka ya mwanzo wa kuanzishshwa kwa umoja huo mwaka 1978.
Tunafuatilia kwa karibu sana kazi za kijana Shaka. Bara na Zanzbar. Amekataa kuwa Mtendaji wa upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano badala yake amekuwa akisafiri huku na huko kupigania maslahi ya Chama, Jumuiya na kuzitetea serikali zote mbili bila kitete au woga.
Shaka amekuwa zaidi ya mwiba kwa Vyama vya Upinzani.Amekuwa akijibishana nao kwa hoja na kufanikiwa kuzima propaganda zao kwa weledi na ujuzi mkubwa kisiasa pengine kuliko kijana mwingine kwenye Jumuiya hiyo.
Siyo siri, amekuwa akisimama nidhamu, miiko na maadili ya uendeshaji wa Jumuiya kwa mujibu wa kanuni na kuheshimu katiba ya ccm .
Shaka amejitahidi sana kuhakikisha sauti ya jumuiya inapigania maslahi ya vijana wenzake na amekuwa akifuatilia masuala ya vijana kwa ukaribu mno kuliko wakati mwingine wowote.
Si hivyo tu, pia amekuwa akilinda rasilimali za Jumuiya na mali nyingine zisitumike hovyo huku akipigana bila hofu pale mashamba ya umoja huo yalipoporwa huko Igumbilo mkoani Iringa na baadhi ya watendaji au wajumbe dhamana wa chama na junuiya ambao wametajwa kujigawia ardhi hiyo na nyingine kuuzwa kwa matajiri kinyume na utaratibu.
Nafikiri ujasiri wake na umakini alionao katika kulinda fedha ma mali za Jumuiya ndiko kunakomponza na kumzalishia maadui wengi wanaoanza kumsakama kwa mambo ya kutunga huku baadhi ya watendaji wenzake wakikiuka taratibu na kuvunja kanuni.
Suala la Igumbilo ndilo linaloonekana sana kumkaba koo Shaka na pengine hata akitakiwa azibwe mdomo na kuzimwa pumzi ili ashindwe kusimamia ukweli na haki za jumuiya. Ninampa pole nyingi.
Hakuna kitu chochote ndani ya Jumuiya kinachokwenda vibaya ila upo ushahidi wa kutosha wapo wanasiasa waroho wa madaraka na wavunja taraibu wameanza kumchimba huku baadhi wakitaka aondoke ili "shamba la bibi" liendelee kuvunwa na kutumiwa kwa israf na viongozi wajanjawajanja kwa hila na utapeli.
Wapo wanadhani wakifanya hivyo watafanikiwa kumdanganya Mwenyekiti na Chama cha mapinduzi ili kuufichua ujasiri na ushupavu wake kisiasa. Yupo mpuuzi mmoja juzi akaandika kwenye mitandao ya kijamii akidai shaka kasamehe milioni 480. Ziko wapi, mbona haonyeshi ushahidi na vielelezo.
Vile vile kwa mujibu wa uendeshaji jumuiya masuala yote yenye utata, tuhuma, ukweli wa mambo na ushahidi wake yanahitaji kujadiliwa kwenye vikao na si mtu mmoja kuropoka barabarani kama wafanyavyo mateja au wapiga debe kwenye vituo vya dsladala .
Kama anavyosakamawa Rais Dk Magufuli na wapinzani uchwara , mafisadi na wapiga dili ni kwasababu tu amekuwa akitaka kusimamia haki, za wanyonge , uwazi, uadilifu na uwajibikaji.Hayo kinadharia nadhani ndiyo yanayomkuta Shaka ndani ya UVCCM kwa wakati huu huku baadhi ya wenzake wakiitaka kuidandia nafasi yake licha ya kwamba anawashinda kiuzoefu na maarifa.
Yule mtu aliyeandika ati shaka anawakumbatia watu wa Lowassa akidhani hilo ndo jungu bovu ambalo litamkasirisha Mwenyekiti wa CCM , nadhami amekawia kuongopa kwasababu uongo wake umekosa mashiko huku shaka akiwa ndiye anayeongoza kumjibu na kumsulubu Lowassa kisiasa pengine kuliko mwanasiasa yeyote ndani ya CCM.
Mapema katika kuanza kwa maandishi yangu kwenye aya za kwanza , nilianza kwa kusema sina ujuzi wa kuandika jambo zaidi ya kuandima barua ya maombi ya kazi .Hivyo basi naomba mnaoisoma muisome kwa utulivu mkubwa na pale itakapoonekana nimekosea chukulieni sina weledi wa kuandika ila nimejikusuru kufikisha mawazo nilionayo kwa kila hatua nilivyoweza kumfuatilia Shaka na ujasiri wake kisoasa ambao sasa unaonekana kumuongezea maadui na kutaka kumkwamisha .
Wenye macho wanamuona, hawezi kuchafuka kwa mizengwe na chuki za kipumbavu za watu wanataka kushika vyeo kwa gharama ikiwemo na kuongopa bila aibu.
Stanley Meshack
SONGWE