Mokes Junior
Member
- Aug 20, 2022
- 7
- 0
PUNDA.
1 Mzigo ukimzidia, haraka anatembea
tajiri humfaidi, jashole kufurahia
hata akijitahidi, atazidi kuumia
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani
2 Viboko anatandikwa, atembee kwa haraka
umauti akifikwa, mzigo upate fika
walah hawezi zikwa, pumziye kikatika
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
3 Vinono anatafuta, makapi wanamlisha
ugonjwa ukimpata, hasira wanazidisha
wakubwa humkamata, mizigo kumbebesha
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
4 Punda na vituko vyake, sijui ndo akiliye
hamtupi bwana wake, humtumikia yeye
hurusha mateke yake, ukimpora mwanaye
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
5 Nyama yake inauzwa, kitoweo wanapata
ngozi yake inamezwa, mashine inachakata
maishaye kuumizwa, maumivu anapata
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
6 Wakimwona anapita, watoto humzomea
lione Punda lapita, limetoka kuumia
njia yake anafata, mawe wakimrushia
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
7 Huku kwetu kijijini, maji hufuata wao
milimani mabondeni, kupanda kushuka wao
je huko kwenu mjini, mnaweza ishi nao
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
8 Bundi afadhali Punda, mchana unapofika
ikilia parapanda, mwituni hawezi toka
masihi alikupanda, hujafa hujasifika
Punda hawezi faidi, jasho lake hasilani.
@MokesJr.