Shairi: Walivyoshindwa kuvila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi: Walivyoshindwa kuvila

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Uloi nga Machi, Jan 26, 2012.

 1. U

  Uloi nga Machi Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WALIVYOSHINDWA KUVILA(FUMBO)

  1. Ninapoamua kula, nakula kitaalamu,
  Sikimbilii mahala,nakula iishe hamu,
  Washindwapo mimi nala, wenyewe wajilaumu,
  Ndivyo nilavyo daima, walivyoshindwa kuvila!

  2. Nakula vilivyolema,washindwavyo binadamu,
  Wapishi hunipa hima, siiogopi lehemu,
  Sistahili lawama,bali sifa kemkem
  Ndivyo nilavyo daima, walivyoshindwa kuvila!

  3. Mlao kijingajinga,mkome kunituhumu,
  Tena muache kiranga,eti kuja nihujumu,
  Ni vema mkajikinga,chakula kuweka sumu!
  Ndivyo nilavyo daima, walivyoshindwa kuvila!

  4. Siombi ninatafutwa,nami sioni ugumu,
  Sisiti nikifuatwa,mguu hutia timu,
  Bure hata nikisutwa,hula nikitabasamu!
  Ndivyo nilavyo daima, walivyoshindwa kuvila!

  5. Kaditamati walaji,mimi si wenu hasimu,
  Ni wenu uzembeaji,katika mastakimu,
  Ndio unipao taji,wapishi wanifahamu!
  Ndivyo nilavyo daima, walivyoshindwa kuvila!

  (Mhadhiri wa Malenga)
  Dar es Salaam


  ,
   
Loading...