Shairi: Wa huba

Shairi: Wa huba

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,508
Reaction score
88,967
1.Huba lako limeniteka, mateka najililia
hakika umenishika, sina pakukimbilia
huba wa mahaba, moyoni najivunia
vuno la mahaba, mwilini nalisikia.

2.Mpenzi wa enzi, nipe pasi kitenzi
mazuzu washenzi, wafumbie utenzi
mimi ndio kenzy, wako wa enzi.

3.Wahuba umenona, hadi wanaumwa homa
singida mpaka dodoma, namba wanaisoma
mtoto unasifika, hata kwenye spika
wanataka uhakika, hawataupata hata kwa gita.

4.Chombezo la hamu, lanipa tabasamu
mzizi wa ufahamu, utakufa kwa hamu
guno lako tamu, mori laufahamu.

5.Binti waruka wewe, godoro lalia kwewe!
unyago walokupa wewe, tuzo lazima wapewe
moja waishika wewe, mbili acha wapendelewe.

6.Usiku umeingia, wachawi wakaribia
milango twajifungia, twende kujilalia
wahuba wanipatia,tunda najilia.
 
Back
Top Bottom