Shairi: Tulikuwa wamoja

Shairi: Tulikuwa wamoja

ostrichegg

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
12,048
Reaction score
6,199
Kweli corona imekita, kudanganya haifai.
Dunia yote walia, hata wenye utajiri.
Wenzetu wanapambana, Siye bado hatujali.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Mlioshika madaraka, hivi mwatupelekapi?
Misingi tumeitoka, twayahama maadili.
Mema tulioachiwa, yanarithiwa na chuki.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Kwa kuringia umwamba, tumesha poteza vingi.
Umoja ulotulea, umekwisha tupwa mbali.
Sasa wapima corona, nao eti wahaini.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Fikra zilizowajaa, kutishana kwa visasi.
Wengine kuwakataa, na kuwazushia uchawi.
Mwanzo wa kushindwa vita, ni dhahiri uko nanyi.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?
 
Chukua tahadhar ,stay home, epuka kudhurura ovyo kama huna issue ya maana kufanya , mwanasiasa hayupo mahala pa maisha yako
 
TULIKUWA WAMOJA

Kweli corona imekita, kudanganya haifai.
Dunia yote walia, hata wenye utajiri.
Wenzetu wanapambana, siye bado hatujali.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Mlioshika madaraka, hivi mwatupelekapi?
Misingi tumeitoka, twayahama maadili.
Mema tulioachiwa, yanarithiwa na chuki.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Kwa kuringia umwamba, tumesha poteza vingi.
Umoja ulotulea, umekwisha tupwa mbali.
Sasa wapima corona, nao eti wahaini.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?

Fikra zilizowajaa, kutishana kwa visasi.
Wengine kuwakataa, na kuwazushia uchawi.
Mwanzo wa kushindwa vita, ni dhahiri uko nanyi.
Pazuri pakipotea, tuje kumlaumu nani?
 
[emoji124][emoji124][emoji124][emoji40][emoji40][emoji40]

Sent using [emoji106]
 
Walimu wa arts ndio maana hamuajiliwi
Majungu sana
 
Chukua tahadhar ,stay home, epuka kudhurura ovyo kama huna issue ya maana kufanya , mwanasiasa hayupo mahala pa maisha yako
Wewe mbona wewe upo nje?
 
Back
Top Bottom