Shairi; Ole wako isinyeshe

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
OLE WAKO ISINYESHE
1)Ni pilipili ya shamba,mjini yawasha nini.
Mjanja nae mshamba,hapa namwacha hewani.
Fumbo nalifunga bamba,usilitie jichoni.
Tutakuhisi ni wewe,ole wako isinyeshe.

2)Mangi kapiga marimba,ukamkaba kooni.
Mtundu kawa mtumba,sasa si kama zamani.
Peku twakanyaga dimba,rafu nyingi uwanjani.
Tutakuhisi ni wewe,ole wako isinyeshe.

3)majembe waliyatupa,wengi wakaja mjini.
Wewe umeshika bapa,wakamata makalini.
Hatujali wewe papa,tutakuvua barini.
Tutakuhisi ni wewe,ole wako isinyeshe.

4)juzi ulipanda ungo,mawe yakashuka chini.
Ni kweli siyo uongo,umeona ukijani.
Eti unapiga zongo,na kuwanga mashambani ?,
Tutakuhisi ni wewe,ole wako isinyeshe.

5)wala usikunje sura,wewe ni wangu mtani.
Walogawana ngawira,wakucheka mtaani.
Hawakuogopi swira,wamezoea,medani.
Tutakuhisi ni wewe,ole wako isinyeshe.

Shairi=OLE WAKO ISINYESHE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom