Shairi; nimekubali

Shairi; nimekubali

Joined
Oct 4, 2023
Posts
50
Reaction score
59
FB_IMG_1745870412622.jpg
NIMEKUBALI

Yanitesa abadani,
Niliyo nayo moyoni,
Naungulia kwa ndani,
Rohoni nina huzuni,
Faraja yangu siioni,
Kufikia huku sikuwahi kudhani,
Wanitesa kwa nini?

Vanessa umebadilika sana,
Wewe wa leo sio yule wa jana,
Ni kweli siku haziwezi kufanana,
Daima hutofautiana,
Sitaki kuibeba hii fitina,
Ukweli mtupu nitaunena,
Niifukuze mbali hii sonona.

Kukupenda nimefanya kosa,
Nd'o maana wanitesa,
Umenionyesha hata nikikupa furaha kwa pesa,
Hutotosheka nami hata ningekuwa Bakhresa,
Hayawi hayawi yamekuwa sasa,
Umeanza kunizushia mpaka visa,
Umebadilika sana Vanessa.

Umejaliwa urembo,
U mzuri wa sura hadi umbo,
Kwangu ukavitumia kama fimbo,
Kuninasa kama chambo,
Kumbe uzuri wako ni fumbo,
Pana lililojaza mengi mambo,
Majibu yake nimeyafata ng'ambo.

Nilipokutangazia upendo,
Ulikubali kwa kishindo,
Ukafanya nibaki lindo,
Nikuoneshe kwa maneno na vitendo,
Simu yangu nikajaza bando,
Wa mapenzi nikautanda utando,
Lakini wewe ukanitupa kando.

Unaleta Isidingo,
Kila siku huishiwi maringo,
Sikuwezi kwenye hizo engo,
Pointi tatu nakupa kwenye huo ulingo,
Unasema hata nikiseti mipango,
Siwezi fikia vyako viwango,
Hata nikishinda bingo.

Eti leo hunitaki,
Wadhibitisha kwa hoja lukuki,
Mara ooo nisikusogelee sipigi mswaki,
Nisikukumbatie na hizi kaniki,
Nikizidi kukusumbua utanishtaki,
Mwanamke kama wewe siwezi miliki,
Siendani na zako kiki.

Sawa mama nimekuelewa,
Kuyafahamu haya nimechelewa,
Nakuombea nyingi baraka uzidi kukirimiwa,
Na bahati zikufuate kama ngekewa,
Utulie upate mme na kuolewa,
Mpate watoto wengi hata mjaze behewa,
Paukwa pakawa!


Limeghaniwa na Kalamu Ya Kabati
 
Back
Top Bottom