Shairi: Nasubiri mropoke

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
NASUBIRI MROPOKE.

1)kinywa cha walo wambea,hakichoki kuongea.
Midomo imelegea,ka mchuzi wa bamia.
Mitani wajikalia,uongo kujipigia.
Mtaja kula makonde,nasuburi mropoke.

2)umbea mmebobea,kwa sifa mwajizolea.
Kusutwa mmezoea,mtaa wa watambua.
Kwangu mkisogea,mawashi nawashushia.
Mateke mtaambulia,nasubiri mropoke.

3)saa ngapi mwajilalia,mchana mwatuwangia.
Kwangu mkija ongea,kibano tawapatia.
Hakyamungu nawapia,sitokuja wachekea.
Jaribuni mtaona,nasubiri mropoke.

4)kabali nitawatia,mapema nawaambia.
Mafua tawakamua,kojo litawatokea.
Zoa mlipo zoea,hapa meno tawang'oa.
Siku yenu itafika,nasubiri mropoke.

5)mbio nitawatimua,enyi msofikiria.
Mwakesha kutusemea,ya watu kusimulia.
Punguza hii tabia,puani yawatokea.
Huu kweli mwaka wenu,nasubiri mropoke.

Shairi=NASUBIRI MROPOKE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
midomo tumepewa,yanini kubania
ropoko twakutolea,moyoni twakuchomea
kimya hakina adabu,utadharau mpaka mababu
heri kukuambia,kuliko kutulipua
 
Back
Top Bottom