Shairi: Mzururaji

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,902
2,000
MZURURAJI

Nenda kote uzunguke
Kapayuke upasuke
Umbea kautangaze
Na taifa uliuze
Wazalendo twasubiri
Kikinuka tukuanze
Mjinga sana ni wewe.

Kijijini una ndugu
Tena masikini sugu
Kula yao hawajui
Nyumba mbavu ya mbwa
Godoro lao busati
Ila wewe kichwa maji
Kutwa kiguu na njia.

Asili yako kiburi
Na tena mtu jeuri
Waache wafe na njaa
Na msiwape chakula
Sababu kumbe ni gumba
Hesabu ulikosea
Sifuri ukaotea.

Uliwatetea ngiri
Ukaona ufahari
Watakuja kukubebea
Ulidhani ni rahisi
Ukahisi ni walevi
Wamekufanya vibaya
Huyo ukadandi ungo.

Endelea kuchafua
Na gaga kulisugua
Huku ni mwendo wa kazi
Maneno hayapo tena
Subiri khamsa tena ije
Ingawa haipo mbali
Urudi usulubiwe.

Mzururaji
Idd Ninga
Arusha,Tanzania
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
134,307
2,000
MZURURAJI

Nenda kote uzunguke
Kapayuke upasuke
Umbea kautangaze
Na taifa uliuze
Wazalendo twasubiri
Kikinuka tukuanze
Mjinga sana ni wewe.

Kijijini una ndugu
Tena masikini sugu
Kula yao hawajui
Nyumba mbavu ya mbwa
Godoro lao busati
Ila wewe kichwa maji
Kutwa kiguu na njia.

Asili yako kiburi
Na tena mtu jeuri
Waache wafe na njaa
Na msiwape chakula
Sababu kumbe ni gumba
Hesabu ulikosea
Sifuri ukaotea.

Uliwatetea ngiri
Ukaona ufahari
Watakuja kukubebea
Ulidhani ni rahisi
Ukahisi ni walevi
Wamekufanya vibaya
Huyo ukadandi ungo.

Endelea kuchafua
Na gaga kulisugua
Huku ni mwendo wa kazi
Maneno hayapo tena
Subiri khamsa tena ije
Ingawa haipo mbali
Urudi usulubiwe.

Mzururaji
Idd Ninga
Arusha,Tanzania
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Nimekuelewa malenga
IMG-20201123-WA0043.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom