Shairi: Mke Mmoja hatoshi

s.crony

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
1,286
458
Mke mmoja hatoshi,sisemi alimradi
Nawala sibahatishi,kama wachimba migodi
Ngoja endezake moshi,ukung'utwe na baridi
Mke mmoja hatoshi,jikusuru na wawili.

Kama utakapo huba,basi ongeza idadi
Taona wakikubeba,haihai kwa sipidi
Utaoneshwa mahaba,ya asmini na udi
Mke mmoja hatoshi,jikusuru na wawili.

Ukenda kwa binti Manzi,chumbachanukia nyudi
Ndanimwe khatui nzi,kwanukia uwaridi
Sisemi kwa Mwanang'azi,kwa mapishi ni stadi
Mke mmoja hatoshi,jikusuru na wawili.

Ni stadi wa mapishi,kitandani si fisadi
Huno wake ushawishi,shuti upande midadi
Ufundiwe hauchoshi,na kumkifu Rashidi
Mke mmoja hatoshi,jikusuru na wawili.

Naupigia mfano,kwa Imamu maulidi
Niimalizie ngano,kwa wake umaridadi
Kimuona yumnono,matilaba afaidi
Mke mmoja haotshi,jikusuru na wawili.

By-Abul Juma Kapera
Mwembe yanga
Temeke
DSM.
 
NI YUPI MKE BORA-By Ally Bakari Almasoud-(Mchanyato);mwalimumchanyato@gmail.com

Kwa utunzi wangu huno,Mchanyato natorora
Nia mnipe maono,ni yupi ni mke bora?
Alowahi fanya ngono,au aliye bikira?
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Siyataki mabishano,nijibuni yenye sura
Niambieni maneno,kwa hoja zenye stara
mwenzenu nina agano,natafuta mke bora
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Nipeni yunu maono,nisije pata hasara
Kwa umbo wote wanono,wazuri pia kwa sura
Kama wana mapatano,wafananavyo ishara
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Huyu alofanya ngono,ni kwa njia ya stara
Ndoa ikawa ndoano,karibu kumpa dhara
Akaitupa mkono,mumewe hakuwa bora
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Usijeleta miguno,mmoja kweli bikira
Huyu binti ni mfano,kwa kuwa yupo imara
Hakuwahi fanya ngono,wala kupata stara
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Chonde sikiza vinono,mwenzako nacha hasara
Ninenayo si kigano,bali ninayo dhamira
Sitaki mke viuno,natafuta mke bora
Kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora?.

Ikiwa uwezekano,nazisubiori bishara
Niyafanye mapatano,nipate mke kisura
Mak'e aliye mnono,tena aliye m'bora
kati ya hawa wawili,ni yupi ni mke bora

-Mchanyato-
 
#@Lawrence Jr....angalia Kiswahili hiki

UMURI WA NYANYA YANGU

Ukati wenda kihaki,tangia zama na tangu
Tuliumbwa mikhilaki,Adamu vyake na vyangu
Nyamahowa mishikaki,kinamo ughafi wangu
Umuri wa nyanya yangu,haulingani na wangu.

Bahari lina kambisi,mijapapa na mingangu
Pungu,pinguso na ngisi,dome,vibua na change
Windo la ngosi na fisi,uchaga kule marangu
Upevu wa nyanya yangu,haulingani na wangu.

Fizile nyanya livivo,ninga na michonge yangu
Amung'una ndivosivo,zanga nabugia zangu
udererewe kitivo,watojela kando yangu
Umuri wa nyanya yangu,haulingani na wangu.

Govile lingasinyaa,chumvi ya tangu na tangu
Enda tata ajikwaa,miundi besera langu
Agwia asa kifaa,mie mbio wanguwangu
Upevu wa nyanya yangu,haulingani na wangu.

Janwale bobo bwabwajo,nalongea shudu yangu
Tega sikiza pambajo,sikizio likomangu
hatufanani utajo,ena tele nna yangu
Umuri wa nyanya yangu,haulingani na wangu

Wisho ufunzi njeraha,etambuza babaangu
Bui lanuka usaha,uganofuavyo kangu
Kingayo mja sitaha,hasanati kiu yangu
Upevu wa nyanya yangu,haulingani na wangu

Arshad Ali
S.L.P 235
Wete,Pemba.
 
Back
Top Bottom