SHAIRI: MAUDHUI: UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI, MASLAHI NA HESHIMA YA MFANYAKAZI

mhugo hantish

Senior Member
Apr 21, 2015
137
36
MAUDHUI: UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI, MASLAHI NA HESHIMA YA MFANYAKAZI.

1* Kokoriko tunawika, kama jogoo wa shamba,
Sauti hizi sikika, watumishi wa muumba,
Mbeleni tumeshafika, Kwanza Mungu twamuomba,
Yale yaliyotuleta, ndio hayo tutasema.
2* kwa makini sikiliza, ujumbe wetu mwanana
Tena bila kupuuza, tumeona ni maana,
VIWANDA kuendeleza, na uchumi kulingana,
Lakini mfanya kazi, haki zake zisirukwe.
3* Kilio cha watumishi, kimepunguza na kazi,
Ya kazi za utumishi, sababu makato hasi,
Yasokuwa faidishi, hapa kazi sio kesi,
Kuendeleza VIWANDA kulenge haki kwa wote.
4* Ajira kwa wahitimu, imekuwa ni hadithi,
Mwaka wote wamedumu, hata hakuna urithi,
Nung'uniko linadumu, hata hakuna urithi,
Kuendeleza VIWANDA, kulenge haki kwa wote.
5* Saa, siku zimevuka, sakata la vyeti feki,
Vyeti feki vimeng'oka, twasubiri kubwa keki,
Sawa Posho zimetoka, mishahara ndogo Koki,
Kuendeleza VIWANDA, kulenge haki kwa wote.
6* Walikopeshwa vizuri, wakasoma wa katoka,
kumi na tano ni ghari, asilimia yatoka,
Sasa shida ni hatari, wasomi kufilisika,
Kuendeleza VIWANDA, kulenge haki kwa wote.
7* Kazi zinapofanyika, Zina mwenye USTADI,
Ila zikiingilika, na wanasiasa bodi,
Uhuru unatoroka, twafanya kazi kwa woga,
Kuendeleza VIWANDA, kulenge haki kwa wote.
8* majigambo, matamko, YANAZIDI kutolewa,
Mengine tija haiko, tunashindwa kuelewa,
Ni wapi hapa tuliko, ama nini twaletewa,
Kuendeleza VIWANDA, kulenge haki kwa wote.
9* Haki za kiutumishi, twaomba zizingatiwe,
Kila yule mtumishi, twaomba apatiwe,
Isiwe ni za kugushi, za halali na apewe,
Tuendeleze VIWANDA, na haki za watumishi.
10* Tulifika kwa kuwika, sasa tunaunguruma,
kama simba kwenye Chaka, akisubiri vinyama,
Mbegu bora twawatika, ikazae himahima,
Tuendeleze VIWANDA, na haki za watumishi.

AINA YA TUNGO: KISASA,
NA Ev Mhugo Hantish
Namba: +255768788303
Email: hantishmhugo@gmail.com
evhantish.blogspot.com
©2017 memory of the past and future events.
 
Back
Top Bottom