Shairi linaloakisi maisha halisi ya leo

N'gwanantugwa

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
347
343
ANDAA CHORUS
MASHAIRI NI SILAHA TOSHA........
USINAKIRI WALA KUKARIRI..
ELEWA DHANA NA TAFSIRI,


picha inakile nachofikiri
Mdundo nausikia kwenye akili
Intro kikatili........


Hatuogopi kusema kwa kuhofia mahakama,
Tutasema mazima bila huruma ama hiyana,
siko tayari kutazama utamaduni unapozama,
Afisa anatafuna kodi yangu naechana.

Wananitisha sitishiki,najiimarisha,
najituma situmiki,kwenye maisha,
Ntahakikisha ukweli nausimisha,
narefusha utamaduni wa maisha ya mwafrika,

Dai la [HASHTAG]#mdaijasho[/HASHTAG] ,jasho kutumika,
Na wachache wanaonyuka,suti zaki Amerika,
Kwa vyeti kutundika,bila maarifa kutumika,
Jasho langu naetafuta kwa dhoruba kwenye nyika,
wanabonya

Nikisema wanasema ni mchochezi wanazima,
Sauti isisike nchi nzima,
Shutuma zitawa andama
ukweli unaposemwa maarifa hujazana,
Kila jicho litaungama na kuungana na,

[HASHTAG]#Wadaijasho[/HASHTAG] acha wale wa libya wa madaso,
au wanasiasa wa kachaso,
Vitwanga moyo akili mwili hawana utakaso,
ubinafsi wameudhihili,bila haya kwenye uso

Huwa sishindwi kuendeleza,kuelekeza
vilaza kuwaeleza kujieleza ni silaha iliyomtoa muingereza,
Kizazi hiki kisingeweza,Babu zetu walichoweza,
kizazi kisichowaza hakitaweza kujikweza
Kizalendo kitakweza umangi meza,Nakusifu mchuzi wa pweza watoto mtaa kuongeza,

Nishtaki unipe hela,
sheria zimelala kichwani siko kifala,
Nachopost kwenye ibara ni haki usichimbe mkwara,
ki [HASHTAG]#diktetauchwara[/HASHTAG] kama yule mzee wa para,niko imara

Kama [HASHTAG]#UKUTA[/HASHTAG] utanikuta siteteleki
hakuna demokrasia kwenye vyama ni unafki na uzandiki,
Hakuna harakati itayoletwa na fisad niiafiki

FULL STOP

@mdaijasho
[HASHTAG]#plateyamaarifanamali[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom