Shairi la "Mo" wetu

donniebrasco

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
887
770
Nina Imani atapatikana,
Mfanyabiashara kijana,
Machoni hajaonekana,
Tunahuzunika sana.

Tunamuomba JALALI,
Sana kwake tunasali,
Atuoneshe hata mahali,
Tuna maumivu makali.

Polisi wetu wanajitahidi,
Na wanaongeza spidi,
Na pia raia wema ikibidi,
Watoe wao ushahidi.

Vikosi vyote viko kazini,
Vinamtafuta juu na chini,
Nchi kavu mpaka majini,
Atapatikana karibuni.

Najaribu sana kufikiri,
Wengi tu ametuajiri,
Lazima ukweli tukiri,
MWENYEZI amsitiri.

Wenzake tunasikitika,
Hatujajua nini kimemfika,
Atalindwa na malaika,
Yeye simba wa Afrika.

Tujaribu kuwa wema,
Tuache hovyo kusema,
Bado sana ni mapema,
MUNGU ni mwema.

Pole kwa wanafamilia,
Waendelee kuvumilia,
Sisi MOLA tunamlilia,
Simba na Yanga pia.
 
Tunaomba apatikane
Yanga na Simba tumuone
Mwenyezi saidia aonekane
Mo watanzania tunakulilia

Simanzi imetushika watanzania
Hatujui uko wali lini utatujia
Wabaya mshindwe kwa mlilodhamiria
Mo watanzania tunakulilia

Utekaji ukomeshwe turudie amani
Serikali zidisha ulinzi wananchi hatuna amani
Kamata watekaji na wasiojulikana jamani
Mo watanzania tunakulilia

Tamati naweka nanga pwani
Nalia kwa uchungu machozi machoni
Nakulilia Mo na wale wote sio hatiani
Mo watanzania tunakulilia
 
Nina Imani atapatikana,
Mfanyabiashara kijana,
Machoni hajaonekana,
Tunahuzunika sana.

Tunamuomba JALALI,
Sana kwake tunasali,
Atuoneshe hata mahali,
Tuna maumivu makali.

Polisi wetu wanajitahidi,
Na wanaongeza spidi,
Na pia raia wema ikibidi,
Watoe wao ushahidi.

Vikosi vyote viko kazini,
Vinamtafuta juu na chini,
Nchi kavu mpaka majini,
Atapatikana karibuni.

Najaribu sana kufikiri,
Wengi tu ametuajiri,
Lazima ukweli tukiri,
MWENYEZI amsitiri.

Wenzake tunasikitika,
Hatujajua nini kimemfika,
Atalindwa na malaika,
Yeye simba wa Afrika.

Tujaribu kuwa wema,
Tuache hovyo kusema,
Bado sana ni mapema,
MUNGU ni mwema.

Pole kwa wanafamilia,
Waendelee kuvumilia,
Sisi MOLA tunamlilia,
Simba na Yanga pia.
Shairi lenye beti 8 namkumbu malenga kipidi nikiwa mdogo
 
Back
Top Bottom