Shairi la kibatari

permist

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
647
405
Ndugu yenu kibatari
Sitaki chenu kiburi
Mlinitupa duhuri
Kwa hiyo yenu ghururi

Na nyingi zenu shururi
Niliweza zisubiri
Nikawa kama kaburi
Wala hamnidhukuri

Mlikuwa mwafikiri
Kuwa mimi ni faqiri
Wapi wenu uhodari
Na ule ujemedari

Nawapeni tahadhari
Kosa msilikariri
Munitundike vizuri
Kwenye uzi wa hariri
Kibatari una nini
Wajisifuni mitaani
Lau kama si sheni
singelitajwa abadani
 
Poleni wazanzibari
Kwa hayo yaliojiri
Mekumbuka kibatri
Japo mlikisahau
 
Walahi Leo ninakiri
Uandishi si kunakiri
Giza limeleta kiburi
Na dawa yake kibatari
 
Myaka ile ya dahari,
Umeme ulipojiri,
Kwa a njia ya bahari,
Wengi mlitahayari,
Kila kona palititiri,
Mwanga ka' magari,
Bila ya kutafakari,
Kwa dharau na shari,
Tena kwa kiburi,
Mkanitupa kibatari,
Bila hata ya hiyari,
Nyuma nikajisitiri,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom