Shairi: Kwaheri mpenzi wangu

Shairi: Kwaheri mpenzi wangu

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
1469733000746.jpg

Kweli safari si kifo, ila yako yaniua,
Inaniua fofofo, mpenzi hilo tambua,
Nenda msalimu Jafo, na wote wano nijua,
Kwaheri mpenzi wangu, nenda urudi salama.

Huu upweke siwezi, sikiza wangu kisura,
Hali yanipa jelezi, hata nishike hasira,
Ewe wangu mkumbazi, sitaishinda subira,
Kwaheri mpenzi wangu, nenda urudi salama.

Kukuaga sina budi, wazee wasubiria,
Usikawie kurudi, ili nipate tulia,
Ukifanya ukaidi, hakika nitajifia,
Kwaheri mpenzi wangu, nenda urudi salama.

Unapolala uote, niko nawe twaongea,
Chakula tukila sote, vitonge wanimegea,
Nikupe ufundi wote, ushindwe kuelezea,
Kwaheri mpenzi wangu, nenda urudi salama.

Nilosema yanatosha, ijapokuwa machache,
Nachelea kukuchosha, na basi lisikuache,
Weye ndiye wanikosha, na wanikome vicheche,
Kwaheri mpenzi wangu, nenda urudi salama.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 Morogoro.
 
Back
Top Bottom