Shairi: Kipato (Income) by; Rugemalira

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
637
KIPATO (INCOME)
Enlarge poem
Kipato wengi hupata, kutunza ndiko kugumu,
Hupata vingi vitita, pesa na vingi muhimu
Bali kutnza utata, watoe zamu kwa zamu,
Kipato wengi hupata, kutunza ndiko kugumu.
Wengi kipato huchota, kuweka hawaeshimu,
Wapatapo hujinata, hudhani wameitimu,
Wenda chezea karata, kamali japo haramu,
Kipato wengi hupata, kutnza ndiko kugumu.
Watu hulia ukata, hawaishi kulaumu,
Jioni utapopita, na kwenye baa chipumu,
Utawaona wapeta, supu ya mbuzi kwa ndimu,
Kipato wengi hupata, kutunza ndiko kugumu.
Mkulima wa ufuta, mahindi kwenye misimu,
Huvuna mengi mafuta, na kufanyia kalamu,
Njaa inapomkuta analia hali ngumu,
Kipato wengi hupaata, kutunza ndiko kugumu.
Wanaume ni matata, matumizi kemkem,
Mishahara wakipata, na posho za kujikimu,
Nyumba ndogo hujikita, pesa zote timtim,
Kipato wengi hupata, kutunza ndiko kugumu.
Ushairi sio vita, ni maneno ya elimu,
Japo unakereketa, ukweli hauwi sumu,
Leo mwami nawasuta, kesho nitawasalimu,
Kipato wengi hupata, kutunza ndiko kugumu.
 
Back
Top Bottom