Shairi: Katiba ya Wananchi

Shairi: Katiba ya Wananchi

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
176
Reaction score
104
attachment.php


Na Nova Kambota,
0712 -544237, Alhamisi, Novemba 6, 2014

Katiba ya wananchi, mwafaka wa taifa
Kuna kucha hakukuchi, isije kuwa maafa
Kuandika ya kukidhi,yahitaji maarifa
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Iokoe wakulima, wavuvi na walemavu
Uchumi ukue hima, iondoe udumavu
Ilinde raia wema, viongozi wasikivu
Katiba ya wananchi , nauliza tutapata?

Watawala watambue, kilio wakisikie
Ukasuku waambae, waikatae ya kale
Machakato uenee, na demokrasi ikue
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Kukaa peke Dodoma,kuichambua rasimu
Kilio cha kina mama, haki zao ni adimu
Ile siku ya kiama, waso haki ni dhalimu
Katiba ya wananchi, nauliza tutapata?

Beti tano nakomea, kalamu naweka chini
Katiba kuongelea,sitachoka ulimini
Tunataka ya kumea, iuondoe uduni
Katiba ya wananchi,nauliza tutapata?
 

Attachments

  • Katiba.JPG
    Katiba.JPG
    26.9 KB · Views: 275
Back
Top Bottom