Shairi: "Kafata Nini Nchini?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi: "Kafata Nini Nchini?"

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Choveki, Dec 4, 2011.

 1. C

  Choveki JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35


  "Kafata Nini Nchini?"
  Nawauliza wajuzi, myajuayo ya ndani
  Alipofika majuzi, akenda hadi chumbani
  Kama vile paka jizi, akivizia machoni
  Kafata nini nchini, kichaka huyo mwajua?

  Nawauliza magamba, kichaka kafata nini?
  Kafika huku atamba, akipepesa machoni
  Kakenua kama mamba, udenda u mdomoni
  Kafata nini nchini, semeni niwe sambamba

  Ama magwanda mwajua?, kilomleta nchini
  Kafika mwachekelea, na ninyi mpo sirini?
  Magwanda mwachemshia, ama mwajua kunani?
  Kafata nini nchini, magwanda naulizia

  Si bure miye nahisi, kufika kwake nchini
  Avizia kama fisi, mzoga u kigamboni?
  Nasaka mwenye nyepesi, atoe hayo ya ndani
  Kafata nini nchini, tujulisheni na sisi

  Kaditama wa tamati, kalamu naweka chini
  Wengine wasema ati, dili la kweli madini!
  Alishawapa visheti, ati sasa taabani
  Kafata nini nchini, tetesi nyingi baruti!

  Choveki


   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  kudos choveki
   
 3. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,920
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  sio 'KAFATA'
  Kafuata. Ok makali?
   
 4. C

  Choveki JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  "Inakubalika"

  Kitunzi yakubaliki, nakujulisha ujuwe

  Kutunga siyo mikiki, kupanga ndiyo kwenyewe

  Tungo ni kama mkuki, misingi uilewe

  Kwa lunga ya kishiri, nasema yakubalika


  Ulizia kwa malenga, magwiji hao wenyewe

  Kinaga tena ubaga, tajua bila kiwewe

  Tunatunga kwa kulenga, fasihi uilewe

  Kwa lugha za kishairi, nasema yakubalika


  Narudi kwake kichaka, namuhisi kama mwewe

  Karuka hadi kafika, nchini yeye mwenyewe

  Ni chepi hicho hakika, anacho taka apewe?

  Kwa lugha za kishairi, nasema yakubalika


  Choveki
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  lugha ya ushairi haina ubaya na uharibifu wa mofolojia za maneno.
  Pengine hata muundo wa sentensi unaweza kuvurugwa ili kufikia kusudi la msanii.
  Sawasawa?
   
Loading...