Shairi hisia zitapita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi hisia zitapita

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mbavu mbili, Oct 29, 2011.

 1. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 804
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  HISIA ZITAPITA...
  Watuita chakaramu,ardhi yetu asili
  Watuvika uharamu,wageni wanowasili
  Matendo yao haramu,wamejawa ukatili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Wageuzwa mahadimu,habithi walojasili
  Wanachumwa kama ndimu,fikra zao zi batili
  Huyu ndiye mwanadamu,mweusi jua hali
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Mahabithi wana damu,dhambi kwao wanajali
  Kheli zama zamadamu,lijitetea kwa hali
  Halafa wanaheshimu,shetani wamfadhili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Najengea ufahamu,sitojivika medali
  Siutaki unajimu, zubaa uachwe feli
  Maisha haya magumu,watuachia pingili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Wamekalia sanamu,machuta hawana hali
  Walamba sukari tamu,makapi kwetu halali
  Ewe mwenyezi rahimu,fungua hizi akili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Rugaruga mwanadamu,ajitoa kwa sabili
  Ishi yao twafahamu,amerika wamejili
  Watuzwa vya hamuhamu,wasahau uasili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia

  Mola aliturehemu,kila kitu cha asili
  Wavitwaa mahasimu,walitutesa mashibli
  Enzi zile zamadamu,alijikania abushili
  Hisia hisia pita,haki itafuatia
   
Loading...