Shairi: Braza soma nyakati


Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,639
Likes
1,043
Points
280
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
2,639 1,043 280
BRAZA SOMA NYAKATI.

1)kubebana na mbeleko,zama zile zimepita.
Mbwa mkali si koko,huyu sasa anang'ata.
Atakuvunja ugoko,ukileta za kuleta.
Braza soma nyakati,zama hizi si mchezo.

2)Atakuchapa na mboko,utalia hutocheka.
Ujinga kwake ni mwiko,ona uvyo tetemeka.
Ulizoea payuko,sasa unaweweseka.
Braza soma nyakati,zama hizi si mchezo.

3)tunaona chozi lako,chini linavyodondoka.
Kisa hizo njozi zako,ndoto zilizopotoka.
Huu sasa muda wako,ingawa tumekuchoka.
Braza soma nyakati,zama hizi si mchezo.

4)sasa una sikitiko,kule wataka kutoka
Ulisema pala pako,vipi leo watoroka.
Ninakupa pole yako,umepata ulotaka.
Braza soma nyakati.zama hizi siyo zile.

Shairi=BRAZA SOMA NYAKATI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 

Forum statistics

Threads 1,273,307
Members 490,351
Posts 30,477,591