SHAIRI: Aliyetuloga Hajafa

SHAIRI: Aliyetuloga Hajafa

Joined
Apr 4, 2016
Posts
68
Reaction score
81
MWAIKENDA
Salaam Bwana Kasinge, nimefika kukuona,
Machache nawe tubonge, mawazo badilishana,
Vipi taifa lisonge? Vijana kibaguana?
Aliyetuloga kafa, vijana twaangamia.

KASINGE
Nami ninakusalimu, karibu wangu rafiki,
Yako mada ni muhimu, tukikwacha unafiki,
Kibaya kwetu na sumu, vijana kwishi kwa chuki,
Mwaikenda wakosea, alotuloga hajafa.

MWAIKENDA
Nelewe yangu kauli, kusema mlozi kafa,
Tupishanapo kauli, sicho kisa maarifa,
Ni misimamo mikali, mapenzi chama ya kufa,
Kasinge unielewe, aliyetuloga kafa.

Kwa nini alishakufa, vibaya twachukiana,
Mtu sipatwe maafa, peana pole hakuna,
Licha sawia taifa, peke vyama vyatukuna,
Kasinge unielewe, aliyetuloga kafa.

Hatunayo maendeleo, uvyama ndiye mchawi,
Chekecha wako upeo, ushirika haukuwi,
Mahasimu kila leo, na matusi yapunguwi,
Maisha pasi umoja, aliyetuloga kafa.

KASINGE
Sana ninakuelewa, hitimisho nabishia,
Mchawi kujielewa, kichwani kwatupungua,
Ushabiki twazidiwa, twafwa pasi kujua,
Alotuloga hajafa, wenyewe hatujelewi.

Mwitwao wakereketwa, hamwezi kubaliana,
Mezani mada kiletwa, lenu kubwa kushindana,
Nzito hoja zikikitwa, mwishoni kutukanana,
Mwaikenda nielewe, alotuloga hajafa.

Haijalishi ni wapi, hata kiwa fesibuku,
Mtaonana makapi, vile mwewe naye kuku,
Shikana kono sa ngapi? Mwekeana marufuku,
Alotuloga hajafa, ni ubongo kutulegea.

Mwenyewe ufikirie, chako chama licho nacho,
Wangapi nihesabie, wasosema kwa kificho,
Mwenyekiti wasijalie, kikovu akiwa nacho,
Alotuloga hajafa, akili haturefushi.

Na matokeo ukada, kilo kwenu kutetea,
Bichwa lajaa husuda, upande ule chukia,
Utegeshi misaada, yenu kesho kuhofia,
Alotuloga hajafa, ufungi ndoa na vyama.

Wale utawasikia, magamba wote kijani,
Na kijani hujibia, lenu chama ukandani,
Vijana mwajimezea, sumu pasi kubaini,
Alotuloga hajafa, wazalendo tubakie.

MWAIKENDA
Yako jamali mawazo, Kasinge nayasikia,
Kile naweka katazo, vyama kujikosea,
Sioni pote katazo, katibani na sheria,
Alotuloga kafa, Kasinge usikatae.

Kimoja nikuulize, karibu ninakuaga,
Zetu kadi tuunguze, ndo wazalendo huwaga?
Na uhuru nieleze, si vyama viliutega?
Kubali ama kataa, aliyetuloga kafa.

KASINGE
Sisemi kadi mchane, si dhambi wala miiko,
Nashauri muungane, kwa ajenda za mashiko,
Mabaya yaonekane, mazuri nayo yaweko,
Aliyetuloga hajafa, tena tunamjua.

Akishaitwa fisadi, sijalishe chako chama,
Mwenyekiti kikaidi, simumunye kumsema,
Kuwasifu huna budi, na wale kifanya vyema,
Alotuloga hajafa, akili zinatupwaya.

Vijana tunatumika, kila panapo umoja,
Kwako kikivurugika, malipo laki moja,
Wona maisha hakika, hujui kesho yangoja,
Alotuloga hajafa, yu hai twaishi naye.

Umoja imara kosa, chama kinakutuma,
Gombea twakupa pesa, kushinda ni lazima,
Usije macho pepesa, wavuruge kundi zima,
Alotuloga hajafa, tumezidi kutumika.

Wenu uchumi kujenga, vyama kando wekeni,
Kasinge yule atunga, nami mwimbaji kwayani,
Pamoja tukijiunga, umasikini kapuni,
Uchumi ushirikyano, alotuloga hajafa.

MWAIKENDA
Huishi katu kunena, Kasinge hapo ishia,
Mekwelewa kwa mapana, tutaja kuendelea,
Naona yawezekana, vijana kubadilikia,
Alotuloga kafa, Kasinge usiku mwema.

KASINGE
Zangu pongezi za dhati, kwako pia Mwaikenda,
Vijana tukaze buti, vyawezekana viwanda,
Serikali yekwe kati, wapi mitaji na randa?
Alotuloga hajafa, usiku mwema bradha.

©2017
barakakasinge@gmail.com
 
Attachments

  • FB_IMG_1728400291628.jpg
    FB_IMG_1728400291628.jpg
    32.3 KB · Views: 15

Shairi la siasa?
 
Imani potofu za kiganga na ushiikina zitawapeleka puta sana msipokua na fikra mpya wala mawazo mbadala dhidi ya mnayoyapitia sasa..

zaidi sana acheni uvivu 🐒
 
We jamaa mchokozi sana... Kulogwa kupo🤭
nawasisitizia tena ndrugu zango MAWAIKENDA na KASINGE

Mambo yamebadilika sana nyakati hizi. Maarifa na bidii katka kazi ni muhimu sana kwa maendeleo yenu binafsi na familia zenu...

Malumbano yenyu ya kinyumbu na kichawa yatawachelewesha sana. Mtalaumiana sana, mtatuhumiana sana na mtalalamikiana sana..

Acheni uvivu,
Acheni imani potofu za kishirikina, uganga, ramli, uchawi, kutoana kafara na kuwachukuana misukule...

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuambatana nanyi MAWAIKENDA na KASINGE, lakin pia wana JF wote 🐒
 
Mbona kama umeumizwa? Unapitia shida gani, mjomba?
 
CCM wanajinafasi watakavyo kwasabb watanganyika ni waoga.

Na hata Tanganyika kukaliwa kimabavu na malkia kutoka nchi jirani ni kwasabb ya uoga na ujinga wa watanganyika.
 
CCM wanajinafasi watakavyo kwasabb watanganyika ninwaoga. Na hata Tanganyika kukaliwa kimabavu na malkia kutoka nchi jirani ni kwasabb ya uoga na ujinga wa watanganyika.
Haloo... Wewe umewaza kwa ghadhabu tena nje ya key kabisa
 
Back
Top Bottom