Shafii daudi acha mbwembe unatukera, jaribu wewe.

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,941
2,251
Nashangaa kuona mtu tena aliyejijengea sifa sana kama Shafii daudi, kila kukicha haishi kuliponda soka la bongo,

unajua watu kama hawa sometimes inageuka kuwa kero kwa sisi mashabiki hasa tunopenda soka letu,

ndio tunajua ni mchambuzi mzuri wa soka, but kuponda sana hakusaidiii kitu, KAMA UNAHISI UNAUWEZO ZAIDI
si utafute timu ufundishe tuone maujanja yako, au KAMA UNAONA UNAWEZA SANA SI KAOMBE NAFASI PALE TFF uwe
mshauri kuliko kila siku kuishia kuwaponda TFF katika vipindi vyenu huko clauds, upate hata nafasi ya ushauri

ndio TFF wanashindwa lakini lazima lazima ukubali ndio effort zao zimefika hapo so wanahitajika wengine zaidi kupanua
wigo wa mawazo.

Hebu cheki wachambuzi wenzako huko ulaya, mbona huwa hawapondi timu zao kama wewe, hebu jaribu kuangalia
ulivyoiponda TANZANIA siku ile zambia ilipochukua UBINGWA WA AFRICA as if wewe si mtanzania bana. yaani mtu unafikia
hatua ya kuapa eti 'TANZANIA HAUTEZI KWENDA KWENYE MICHUANO MIKUBWA LABDA ITOKEE WASHIRIKI WAPATIKANE KWA
KURUSHWA SHILINGI'

TUWEKE UZALENDO MBELE BWANA, KAMA MNAWEZA SI MTUSAIDI WABONGO KULIKO KUPONDA NA KUFAGILIA YA ULAYA!!!!! HAISAIDII KITU
 
Dah, Ni Kweli lakini ungekuwa wazi kutoa yale ambayo anayoponda ili wachangiaji wengine washiriki vizuri maana clouds sio inasikika sehemu zote.
 
wabongo ndivyo tulivyo huwa tunaponda sana vya kwetu na kushabikia vya nje!!! wapo wengi tu kina shafii!!! wanaishia kuwa na porojo nyiiiingi zisizo na maaana.

THIS IS THE TIME FOR ACTION ......! hatutati porojo
 
Yule mwandishi aliye kuwa anaponda tff si kala bata pale tff nae anafanya nn cha maana pale?
 
Dah, Ni Kweli lakini ungekuwa wazi kutoa yale ambayo anayoponda ili wachangiaji wengine washiriki vizuri maana clouds sio inasikika sehemu zote.
Jamaa alichoponda ni kuwa viongozi wa soka tanzania wanapindisha sheria so haiwezi songa mbele
 
Jamaa alichoponda ni kuwa viongozi wa soka tanzania wanapindisha sheria so haiwezi songa mbele

ndio kama wanapindisha sheria, si aombe nafasi pale tff apate ili yeye anyooshe, kuliko kuishia poroja ambazo hazina effect yoyote katika maendeleo ya soka
 
Humu jamvini watu wengi tu tanakosoa mambo mbalimbali lakini haimaanishi kuwa wote wanaokosoa wanaweza kuongoza taasisi hizo, hiyo haiwazuii kusema kasoro wanazoziona. Naamini hivyo hivyo kwa mpira. Ni wakati vilevile waTanzania tujue kuwa uzalendo siyo kutokukubali ukweli. Ni kujidanganya nafsi zetu kuamini kuwa uendeshaji wa soka letu kuanzia ngazi ya chini mpaka TFF unaweza kutufikisha mbali.
 
kuna mambo anayojadili Shafii Dauda nayakubali kama klabu kuanzisha kamati ya ligi lakini mbwembwe zimezidi wakati wa kuripoti hasa mechi za kimataifa kabla mtu ajataja matokeo umesharukia kuanza kuchambua tangazeni matokeo kwanza uchambuzi uje baadaye ni kweli mbwembwe zimezidi ila kuhusu kamati ya ligi kwa vilabu nakuunga mkono
 
Lazima mfahamu role ya kila mmoja kwenye football industry. Huwezi kusema kuwa Shaffih akafundishe timu kwa kuwa ameponda soka lao, thats foolish argument.
Shafih ni analyst, anaeleza kile chenye anakiamini, na kiasi kikubwa yuko sawa. Uzalendo sio kufunika kombe mwanaharamu apite, ila ni kushughulikia yale ambayo football analysts wanakikosoa. For that reason, TFF na viongozi wa Simba na Yanga ndio hawana uzalendo. Halafu, why only Dauda? Karibu wachambuzi wote wa soka, Riky, Edo, Maestro, Momburi na hata Osiah Anjetile wakati akiwa na Mwananchi Comm, wamewahi kuponda soka letu mara za kutosha tu. Halafu nilishawahi kumsikia Dauda akimsifia Ngassa alipoenda kufanya majaribio na Seatle Sounders, hata alisafiri kwenda Marekani kumwona akicheza game v/s Manchester United.
Fikiria tena mkuu!
 
wabongo si ndo tulivyo...! kuona wenzako wanafanya vibya

Huyu Hosea alikuwa mwandishi wa gazeti alikuwa anaponda sana TFF pamoja na Maximo sasa Tenga wakampa ulaji alete fikra mpya tunaona timu ya Taifa ndo kwanza inazidi kudidimia kila kukicha molali hakuna rank ya fifa tunazidi kuporomoka
 
hilo ***** tu ..hata uandishi wake wa habari sijui kasomea wapi
 
Lazima mfahamu role ya kila mmoja kwenye football industry. Huwezi kusema kuwa Shaffih akafundishe timu kwa kuwa ameponda soka lao, thats foolish argument.
Shafih ni analyst, anaeleza kile chenye anakiamini, na kiasi kikubwa yuko sawa. Uzalendo sio kufunika kombe mwanaharamu apite, ila ni kushughulikia yale ambayo football analysts wanakikosoa. For that reason, TFF na viongozi wa Simba na Yanga ndio hawana uzalendo. Halafu, why only Dauda? Karibu wachambuzi wote wa soka, Riky, Edo, Maestro, Momburi na hata Osiah Anjetile wakati akiwa na Mwananchi Comm, wamewahi kuponda soka letu mara za kutosha tu. Halafu nilishawahi kumsikia Dauda akimsifia Ngassa alipoenda kufanya majaribio na Seatle Sounders, hata alisafiri kwenda Marekani kumwona akicheza game v/s Manchester United.
Fikiria tena mkuu!

Mimi naamini Shaffii anatoa maoni kama mtu mwingine yeyote, hata mimi huwa naponda TFF nyakati fulani ni kwa sababu sometimes inaendeshwa kihuni mno, na msingi wa kuendeshwa kihuni ni vile tu uingiaji wa madarakani unatawaliwa na fitina nyingi,
 
ifike kipindi kanuni za FIFA zibadilike.
Serikali iwe na mamlaka ya kuingilia utendaji wa chama cha soka, since chenyewe kiko chini ya serikali na kinaendeshwa kwa kodi za wananchi. Kile kipengele cha kutoingiliwa katika maamuzi ndio kinawapa kiburi, otherwise wajiendeshe kwa funds kutoka huko huko FIFA.
Kuhusu Shafih, mtoa mada anaendeshwa na hisia binafsi, hata mimi kuna vitu Shafih ananikera, kama suala la kutoa takwimu na taarifa za uwongo, lakini si suala la kuiponda TFF.
 
mi sioni tatizo lake ni nini,acha aseme kile anachokiamini,na ni ukweli soka la bongo ni michosho 2.
 
Back
Top Bottom