Shabaha ya Maendeleo ya Nchi

Shabaha ya Maendeleo ya Nchi

Joined
Nov 8, 2013
Posts
33
Reaction score
28
Shabaha ya kufikia maendeleo bora, sahihi na kweli ni dhana ya kila Mtanzania, na yeyote mwenye mapenzi mema na Tanzania. Maendeleo haya ili kuyafikia ni lazima kila mmoja katika umoja ashiriki kikamilifu kwa namna mbalimbali kwa kadiri ya uwezo wake. Kumbe, kujenga nchi si suala la mtu mmoja bali ni jamii nzima. Wivu, uvivu, ubinafsi, uchoyo, ufidhuli na uhaini ni maadui wakubwa dhidi ya maendeleo haya. Sasa umefika wakati wa kufunguka kifikra ili kuweza kuona mbali kwa ueledi na uakinifu wa hali ya juu. Kulalamika lalamika bila ya kufanya mabadiliko chanya si jambo la kiungwana. Mtanzania wa kweli tutamjua kwa upendo alionao dhidi ya nchi yake Tanzania. Utanzania ndiyo fahari yetu.
 
Back
Top Bottom