Hussein J Mahenga
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 753
- 659
Leo tumezindua ujenzi wa reli ya mwendokasi (Standard Gauge Railway) ambao sasa unafanya idadi ya vipande kufikia viwili ukijumlisha na kile cha kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro. Reli hii imetajwa kuwa na mengi mazuri ikiwa ni pamoja na:
Treni za mwendokasi zimeanza kuwepo tangu miaka ya 1800, yaani karne ya 19, sawia na miaka mia mbili iliyopita. Sisi tunajivunia tu hii ya sasa na tunatarajia maendeleo, Marekani kwa mara ya kwanza imejenga reli ya kiwango cha kimataifa, yaan Standard Gauge Railway au wao walikuwa wakiita Stevenson Railway mwaka 1831 (New York-Erie Railroad) na kuanza kutumika rasmi mwaka 1845. Pamoja na maendeleo hayo ya awali kabisa ambayo leo hii sisi twatamba nayo, Marekani iliingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe (civil war) mwaka 1861 hadi 1865. Sababu ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa ni ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia hasa kwa wamarekani weusi, na hasa katika mgawanyiko wa uchumi.
Uingereza, kwa mara ya kwanza reli za kiwango cha kimataifa, SGR, zilijengwa miaka ya 1830, tena ni zaidi ya moja. Kwa mfano, The Killingworth Colliery Rail, The Hetton Colliery rail na The Stockton and Darlington rail zilijengwa mwaka 1821, 1822 na 1831 sawia. Lakini mwaka 1848 kulikuwako na mapinduzi kibao yaliyojulikana kama The Revolutions of 1848 ambapo waliberali walishiriki mapinduzi ya kuuondoa utawala wa kifalme na kuweka utawala wa kidemokrasia ingawa hadi sasa hapakuwa na mafanikio kama yaliyotarajiwa.
Afrika Kusini, reli za mwendokasi zilijengwa miaka ya 1900, na mfano mzuri ni reli inayounganisha Capetown na Johannesburg ambayo ilijengwa mwaka 1914. Lakini hadi sasa, na hata baada ya kupata uhuru wao na kuondosha utawala wa kibaguzi, Apartheid rule, mwaka 1994, bado wanataka demokrasia.
Leo kwenye uzinduzi wa treni yetu ya mwendokasi, naona vitisho vimetawala kuanzia kwa wasaidizi wa rais hadi rais mwenyewe. Kauli ni moja tu kwamba, hatutamvumilia mtu yeyote ambaye analenga kuharibu na kuharibu maana yake ni kupinga ama kuandamana, kwa muktadha wa maneno haya.
Labda tuelewane jambo moja. Watanzania wanachotaka ni uhuru wa kweli na demokrasia madhubuti. Kuwafurahisha kwa reli ya mwendokasi na kutaka kuwaziba midogo wasiongee ni utumwa, na ndiyo hoja yangu hapa. Hata kama watakuwa na reli ya mwendokasi, lakini kama hawana uhuru wa kumkosoa ama kuwakosoa viongozi wao, basi haina maana hata kidogo ya kuwa na hiyo reli, kwani hakuna maendeleo ya aina yoyote zaidi ya utumwa. Unafikiri ni kwa nini watu walifanya mapinduzi na kuingia vitani Marekani, Uingereza na nchi zingine kadha wa kadha? Demokrasia.
Tukiwa tunashangilia kuwa tunajenga reli kwa kiwango cha kimataifa, tusisahau kuwa Ben Saanane hadi leo hayupo. Unafikiri wazazi wa Ben Saanane wataitumia reli hiyo kwa amani? Tunapojipambanua kuwa sasa tunajenga reli kwa kiwango cha kimataifa, Binti Akwilina hayuko tena nasi, kakatishwa ndoto na vyombo vya ulinzi vyetu. Je, wazazi wa Akwilina wataitumia reli hiyo kwa amani? Tunapoongea kujenga reli ya kiwango cha kimataifa, Lissu anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji kwa kushambuliwa kwenye nyumba za serikali zinazolindwa masaa 24 kwa siku. Hakuna uchunguzi unaoendelea juu ya tukio hilo ama kauli yoyote, lakini tunatamba na reli ya kiwango cha kimataifa. Je, familia ya Lissu itatumia reli ya kiwango cha kimataifa kwa amani?
Watanzania, kabla ya kuwa na reli ya kimataifa, tunahitaji kwanza kuwa na demokrasia imara. Tusidanganyike na maneno mepesi kusema kuwa reli hii itakuwa na manufaa kwa watanzaia wote, pasi na demokrasia, nawaambieni tunaingia utumwani. Tunahitaji demokrasia. Tunahitaji utawala bora. Tunahitaji siasa safi. Tunahitaji uhuru wa kujieleza na uhuru wa kupata habari bil mipaka.
Uncle Kaso
14.03.2018
- kuzalisha ajira, ambapo katika uzinduzi wa leo tumepewa takwimu kuwa, kuna kadirio la ajira takribani laki sita kwa watanzania kwenye ujenzi huu. Jumlisha na ajira zingine elfu kumi, au hata na zaidi, kwenye ujenzi wa bomba la mafuta ghafi (crude oil pipeline) la Tanga-Hoima, na;
- kurahisisha usafiri na usafirishaji mizigo kwa watanzania ambapo inakadiriwa kuwa, mara tu itakapokamilika, treni hii ya umeme itakuwa na mwendokasi wa km/saa 160. Kwa hiyo, kama Mbunge wa Dodoma Bw. Mavunde na Rais mwenye walivyosema, mfanyabiashara wa mchicha wa Ihumwa pale Dodoma ataweza kusafiri kupeleka mchicha wake Dar, atasalimia ndugu zake na kisha kurudi Dodoma na pengine kula chakula cha mchana kwake Dodoma.