Mijadala ya makadirio ya bajeti ya wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi inaendelea kwa siku ya pili hii leo.
Wabunge wengi waliopata nafasi ya kuchangia kwenye bajeti hii wameona kuna haja ya tume kuundwa itakayoangalia mustabali wa elimu yetu kwa ujumla kwani kutokana na mfumo wa elimu tulionao kwa sasa ni dhahiri kuwa tunawandaa wataalam feki wa kisasi kijacho.
Wengi walipendekeza maslahi ya waalimu yaboreshwe ili wale wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi wapelekwe kwenye vitivo vya elimu ili wawe waalimu tofauti na sasa ambapo wanaoonekana kuwa na ufaulu wa chini ndio wanaopelekwa kwenye vitivo vya elimu. Akionyesha jinsi elimu yetu ilivyokuwa mbovu kwa sasa mbunge wa jimbo la Kigoma mjini ndugu Peter Serukamba alisema wakati wa mchango wake bungeni jana kuwa asilimia zaidi ya 60 ya wanafunzi wanaosoma shahada ya pili hapa nchini wanaandikiwa 'thesis' kwa maana ya kuwa hawana uwezo kabisa.
Niliposikia hivyo nikakumbuka madai ya watu wengi kwenye mitandao ya kijamii kuwa mheshimiwa mmoja mwenezi wa chama cha zamani amemaliza shahada yake ya pili mzumbe kwa kusaidiwa kuandikiwa dissertation yake.