Seriously, "Who're You"? Eti Anauliza!

Seriously, "Who're You"? Eti Anauliza!

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
19,538
Reaction score
26,190
Kawaweka ma-'Rear Admiral' (ulisha waona lakini?); majenerali anaowaamini yeye kwenye sehemu za jeshi akilenga kumbana kikaragosi alichokiweka kama maonyesho kwenye nafasi ya juu ya jeshi, na hapo kajiaminisha kuwa anaweza kusema mbele za wazee wachovu kwamba nchi anayoiongoza yeye ni nchi huru; na kupigiwa makofi na hao wanaomsikiliza!

Tatizo lake ni kwamba, hajui maana ya nchi kuwa huru ni nini. Na kwamba, uhuru wa nchi yoyote unalindwa na umoja wa wananchi wa nchi hiyo, kwanza; jeshi linawategemea wananchi kufanikisha kazi yake ya kulinda mipaka ya nchi na usalama wake kwa jumla.

Kwa hali aliyoitengeneza Samia Suluhu Hassan hapa nchini, haihitaji hao watu anaowahoji wao ni kina nani, kujuwa uwezo wao wa kumtoa madarakani na kusambaratisha Genge zima.

Hao watu wakitaka, ni kutoa vifaa tu, bila ya ushiriki wao moja kwa moja; hapo atapata jibu analotafuta.

kama yeye kahakikishiwa na wajomba zake kuwa watamlinda na kuifanya Tanzania iwe Sudan nyingine; hilo pia asilisahau.

Samia ni mbumbu mbumbu hasa!
 
Wazee wale wakapiga makofi na kusimama, kwa mtu ambaye anajisifia kwamba nguvu iliyotumika kuuwa maelfu ya watu ilikuwa ni sawa tu,
 
Kwamba hajui maana ya uhuru, acha utani bwashe! Kumbuka ana pointi 5 ya Civics. Kiswahili tu ndio aliteleza akapata pointi 4.
 
Unategemea 'akili' ipi kwa mtu aliyefanikiwa kupata D moja tuu tena ya kiswahili kwenye matokeo ya form 4?!.
D moja tu tena ya Kiswahili duuh kuna mzee nimemwambia hilo ananiambiaa elimu haina issue nikashtuka sana elimu haina issue..?
 
Back
Top Bottom