MLUGURU
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 2,836
- 3,539
Hii stand ya makumbusho imekuwa ni kiungo muhimu cha usafiri kuelekea sehemu mbalimbali za mji huu Dar es Salaam.
Lakini kinyume na umuhimu wake naona imesahauliwa kabisa kwani maendeleo ya miundombinu ndani ya jiji hili ni tofauti kabisa na miundombinu ndani ya stand hii muhimu.
Mashimo makubwa yaliyo ndani ya stand hii ni hatarishi kwa usalama wa magari ya wafanyabiashara mbalimbali ambao kwa sasa ndio walipakodi wakubwa katika serikali hii ya awamu ya tano.
Madereva wa mabasi makubwa aina ya Tata na eicher imekuwa mtihani mkubwa kwao kutoka na abiria salama bila kupata hitilafu yoyote katika magari hayo.
Leo nimekuwa shuhuda wa basi aina ya tata linalofanya safari zake Mbagala- Makumbusho likivunja sijui ni spring au kitu gani na hatimaye kushusha abiria wake.
Ombi kwa serikali hii ya sasa iangalie kwa jicho la tatu hii stand kuanzia waliosimamia ujenzi wa stand watuambie imekuwaje stand hata miaka 5 haijafika imechoka hivi?
Kifupi leo nimewaonea huruma sana wafanyakazi kwenye lile basi.