Serikali Zanzibar yakaliwa kooni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Zanzibar yakaliwa kooni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Apr 27, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]

  na Chalila Kibuda

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]CHAMA cha TADEA (Zanzibar) kimesema bado hakina imani na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu msimamo wake wa kuwawajibisha watumishi na viongozi waliohusika kuuza kinyume cha taratibu, majengo ya Mambo Msiige na Starehe Club yaliyoko Mtaa wa Mjimkongwe visiwani humo.

  Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Ali Khatibu, akizungumza na Tanzania Daima kwa simu, alisema haitoshi serikali hiyo kurudishiwa pesa tu bila waliohusika kupelekwa mahakamani kujibu mashitaka hayo, kwani tayari tume iliyoundwa na serikali imebaini makosa mengi ikiwa ni pamoja na kukiukwa kwa taratibu na sheria ya manunuzi.

  Kauli ya TADEA imekuja siku chache tangu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itoe tamko lake juu ya sakata hilo ambapo imependekezwa kuwa wale wote waliohusika watawajibishwa kulingana na taratibu za kisheria.

  Alisema bado serikali hiyo haiko makini kutokana na kupuuza ushauri uliotolewa hapo awali kuhusu sakata hilo, jambo ambalo lilisababisha kuundwa kwa tume ambayo ilibaini kuwa majengo ya Mambomsiige na Starehe Club zilimokuwa ofisi mbalimbali za serikali hiyo kuhamishwa baada ya majengo hayo kuuzwa.

  "Wananchi wa Mjimkongwe na Wazanzibari wote tulipinga vikali hatua hiyo lakini serikali haikujali na badala yake tuliamua kuliandikia Shirika la UNESCO na ndipo tumeanza kuona hatua zikichukuliwa," alisema.

  Baadhi ya ofisi hiyo ni pamoja na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Mrajis Mkuu wa Serikali, Shirika la Meli Zanzibar na Mahakama ya Kazi Zanzibar ambazo zimelazimika kuhamishwa baada ya mwekezaji Kampuni ya Kempinski Group Hotel kulikodisha jengo hilo kwa shilingi bilioni mbili (2.25.0 kwa muda wa miaka 99.

  Katika kikao cha Baraza la Mapinduzi kilichomalizika wiki iliyopita ilipendekezwa kuwa majengo hayo yote yarejeshwe serikalini na iwapo itaonekana bado kuna ulazima wa kuyakodisha zoezi hilo lifanyike kwa kufuata taratibu na sheria za uwekezaji kwa masilahi ya taifa.

  Akiahirisha Baraza la Wawakilishi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd aliwataka viongozi wote waliohusika kwenye sakata hilo kujitoa serikalini haraka iwezekanavyo ili kuiepusha serikali yake na aibu ambayo inaweza kuipata mbele ya jamii.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe, Issa Malani aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari kuwa Kampuni ya Kempisk imekabidhi ramani mbili za mradi huo na mamlaka imeshindwa kuzipitisha kwani hazikukidhi sifa za uhifadhi wa Mji Mkongwe.

  Majengo hayo yaliyopo kwenye eneo hilo lililokodishwa yalikuwa yanamilikiwa na Wizara ya Makazi, Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi.

  Vyama vya TADEA, AFP na NCCR- Mageuzi visiwani humo viliitisha mkutano wake na vyombo vya habari mwaka jana na kueleza wazi kuwa uuzwaji wa majengo pacha ya Serikali ya Zanzibar haukufuata sheria ya manunuzi namba 9 ya 2005. Hata hivyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilipuuzia malalamiko hayo mpaka vyama hivyo vilipoandika barua kwa Shirika la kimataifa la UNESCO kulalamikia jambo hilo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania inaongoza viongozi wake kwa ufisadi wakutisha wa mamilionea , kwa umaskini katika nchi maskini watu wake tanzania ni moja wapo, swali jee rasilimali za nchi kweli tanzania inastahili kuwa nchi maskini?
   
Loading...