Serikali Zanzibar yabanwa ukodishaji majengo ya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Zanzibar yabanwa ukodishaji majengo ya umma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi Wetu - Majira

  SAKATA la ukodishwaji wa majengo ya kihistoria katika mji Mongwe Zanzibar, limeingia hatua mpya baada ya Kampuni ya Uwakili visiwani humo kuiandikia serikali
  barua ya kusudio la kuishitaki kwa madai ya kuyakodisha kinyume na sheria ya manunuzi ya mali za umma na. 8 ya mwaka 2005.

  Barua ya Aprili 21 mwaka huu ya kusudio la kuishitaki serikali kutoka kampuni ya uwakili ya A.J.J.O JUMA Esquire inampa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe Zanzibar siku 21 kubatilisha mkataba wa ukodishaji majengo hayo.

  Kampuni hiyo ya uwakili ambayo inawakilisha wananchi wa Zanzibar inasema katika barua yake hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa viongozi wakuu wa serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuwa sheria zimekiukwa kwa kuwa mwaka 1964 wakati serikali ilipotaifisha ardhi, eneo la Mambo Msiige lilikuwa moja ya maeneo yaliyowekwa chini ya umiliki wa umma.

  Madai mengine ni kwamba wananchi wa Zanzibar hawakuhusishwa katika kukodisha majengo hayo ya kihisitoria ambayao yamekodishwa kwa ajili ya ujenzi wa hoteli ya kitalii inayotarajiwa kujengwa na kampuni ya Zamani Zanzibar Kempinsk.

  Awali kampuni hiyo ilimwandikia kusudio la kushitaki Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu suala hilo. Barua hiyo ya Aprili 13 mwaka huu ikitaka wananchi wa waelezwe bayana iwapo sheria zilifuatwa katika kuingia mkataba huo.

  Wakati sakata hilo likiendelea, wakazi 200 wa Zanzibar wiki hii wameorodhesha majina yao wakipinga kukodishwa kwa majengo hayo kwa madai kuwa hawakushirkishwa kama sheria inavyosema.

  Wakiwa wameandikishwa majina na saini zao, wananchi hao katika tamko walilolitoa wanataka mkataba huo uvunjwe na wapewa fursa muafaka ya kutoa maoni yao kuhusiana na mkataba wa ujenzi huo.

  Wanapinga pia hatua ya serikali kubandika tangazo kwenye eneo la majengo hayo lilimtaka mwananchi yeyote mwenye maoni kuhusiana na ujenzi huo kuyawasilisha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.

  Hata hivyo utata ulioko kwenye tangazo hilo ni kwamba liliandikwa Aprili 8 mwaka huu lakini likabandikwa ukutani Aprili 19 mwaka huu huku likionesha kuwa kazi ya kutoa maoni inatakiwa kumalizika nda=ni ya wiki tatu.

  Wananchi wanadai kuwa utata huo wa tarehe umepangwa makusudi ili kuwanyika fursa ya kutoa maoni hasa ikizingatiwa kuwa siku siku takribani sita zilimezwa kwenye sikukuu za mapumziko ya Pasaka na sherehe za Muuungano.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Safi sana.

  Wananchi lazima wachukue hatua wenyewe pale wanapoweza.
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ufisadi kama huu zanzibar ni kitu cha kawaida kabisa.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa Muungano Ukivunjika Ufisadi kama huu Utakuwa Mkubwa?
   
Loading...