Serikali za Umoja wa Kitaifa: Ndicho wanachotaka CHADEMA?

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Wasalaam,

Kumekuwa na wimbi la uundwaji wa serikali za Umoja wa Kitaifa kwa nchi za Afrika siku za karibuni. Serikali ya Umoja wa Kitaifa siyo kitu kigeni ila kilicho kigeni ni sababu mpya ya uundwaji wake. Sababu kuu iliyokuwa inasababisha uundwaji huo inapatikana katika maneno yafuatayo;

.....Here the opinion has taken root that in times of crisis - political, military or economic - we must unite under such a government. The argument is that in times like these, there is no room for petty political differences and we must all make a common effort to overcome the causes of the crisis.......

"
Tough opposition is vital to democracy" By Hillel Schocken.

Kwa maneno hayo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa muundo wake unazaliwa wakati wa crisis it be political, military or economic.

Kwa sasa hivi Serikali hizo zinaundwa wakati wa crisis za uchaguzi zinazosababishwa na walioshindwa kupinga matokeo au waliokuwa madarakani (Kenya na Zanzibar) kukataa kuachia madaraka (angalia Zimbabwe na mawazo ya wachache kuhusu suluhu ya Ivory Coast). Pia vilevile uundwaji wake unaweza ukapangwa way before the crisis kama ilivyo Zanzibar. Kwa Zanzibar makubaliano yalifikiwa wakati ambao crisis 'ilishamalizika' kwa lengo la kuzuia machafuko baada ya uchaguzi wa 2010!! Mtu utajiuliza, je uchaguzi ule ulikuwa na maana gani? Lengo lilikuwa ni kushiriki kukamilisha utaratibu au ni kutoa nafasi ya demokrasia ya kweli? Hilo naaliachia hapo kuzua mjadala endelevu.

Matunda ya muundo huo sio lazima yawe umoja wa kitaifa (angalia Kenya). Hillel Schocken anasema "one must distinguish between the concept of "national unity" and a national unity government. A national unity government is no guarantee of national unity"

Leo asubuhi nimesikia Tunisia wataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ndipo nikajiuliza, je CHADEMA na wao wanataka Serikali ya Umoja wa Kitaifa? Ndio kilichochochea uamuzi wa kuandamana Arusha ili kucreate crisis?

Je ni faida zipi zipatikanazo kwa uundwaji wa Serikali za Umoja wa Kitaifa? Serikali hizo ni kwa manufaa ya viongozi au wananchi? Ni yapi wananchi wa Zimbabwe, Kenya, Zanzibar n.k wanaweza kufurahia kwamba yameletwa na Serikali za Umoja wa Kitaifa?

Je ni mfumo ambao Tanganyika tunaweza kuufuata hivyo CHADEMA waanzishe vurugu CCM wakatae kuachia madaraka. Wengine wachochee udini na ukabila ili tuvurugane mwishoni tuunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa???

Nawasilisha!!:sing:
 
Nawasilisha!!:sing:[/QUOTE]
umwtumwa na MAKAMBA, chama tawala ndicho huanzishaga vurugu kwa kuwa kinaitumia dola vibaya kama ilivyotokea Arusha na Kenya.HATUTAKI IWEPO SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA BARA? nani ataikosoa serikali if CDM watakuwa part ya Gvt? in GNU CCM hawana uwezo kiutendaji itabidi wabwbwe na CDM kwa hiyo kumpa CDM mzigo usiostahili.Kila chama kitawala peke yake (rais na mawaziri) tukipime kivyake sio mambo ya RAILA na MWAI.
 
Hayo yoooote umeyato wapi mkuu!! Pole lakini uajaribu kweli kuwasilisha ila wasilisha kama muelewa
 
Tatizo la kusoma heading halafu unakimbilia kwenye 'reply topic'.

"WISE MEN TALK BECAUSE THEY HAVE SOMETHING TO SAY; FOOLS, BECAUSE THEY HAVE TO SAY SOMETHING"

hayo si maneno yangu nimeyakuta humuhumu!! Sasa sijui nani anatakiwa ayasome!!

Na kwanini mtu awe muoga kutafakari kinachosemwa? Kwanini usipinge kwa hoja badala maneno makali yasiyo na ulazima kutumika.

Hoja iliyopo mezani ni kuhusu vurugu na uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Inawezekana wewe hutaki wenzako wanaitaka. Au wewe unaitaka wenzako hawaitaki. Ndio maana ya mjadala. Unaweza kutoa hoja yako "CHADEMA haitakubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa" ambayo utaipenda wewe pamoja na wengine wanaopenda kusikia na kusikiliza mazuri siku zote!!
 
Wasalaam,

Kumekuwa na wimbi la uundwaji wa serikali za Umoja wa Kitaifa kwa nchi za Afrika siku za karibuni. Serikali ya Umoja wa Kitaifa siyo kitu kigeni ila kilicho kigeni ni sababu mpya ya uundwaji wake. Sababu kuu iliyokuwa inasababisha uundwaji huo inapatikana katika maneno yafuatayo;

.....Here the opinion has taken root that in times of crisis - political, military or economic - we must unite under such a government. The argument is that in times like these, there is no room for petty political differences and we must all make a common effort to overcome the causes of the crisis.......

"
Tough opposition is vital to democracy" By Hillel Schocken.

Kwa maneno hayo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa muundo wake unazaliwa wakati wa crisis it be political, military or economic.

Kwa sasa hivi Serikali hizo zinaundwa wakati wa crisis za uchaguzi zinazosababishwa na walioshindwa kupinga matokeo au waliokuwa madarakani (Kenya na Zanzibar) kukataa kuachia madaraka (angalia Zimbabwe na mawazo ya wachache kuhusu suluhu ya Ivory Coast). Pia vilevile uundwaji wake unaweza ukapangwa way before the crisis kama ilivyo Zanzibar. Kwa Zanzibar makubaliano yalifikiwa wakati ambao crisis 'ilishamalizika' kwa lengo la kuzuia machafuko baada ya uchaguzi wa 2010!! Mtu utajiuliza, je uchaguzi ule ulikuwa na maana gani? Lengo lilikuwa ni kushiriki kukamilisha utaratibu au ni kutoa nafasi ya demokrasia ya kweli? Hilo naaliachia hapo kuzua mjadala endelevu.

Matunda ya muundo huo sio lazima yawe umoja wa kitaifa (angalia Kenya). Hillel Schocken anasema "one must distinguish between the concept of "national unity" and a national unity government. A national unity government is no guarantee of national unity"

Leo asubuhi nimesikia Tunisia wataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ndipo nikajiuliza, je CHADEMA na wao wanataka Serikali ya Umoja wa Kitaifa? Ndio kilichochochea uamuzi wa kuandamana Arusha ili kucreate crisis?

Je ni faida zipi zipatikanazo kwa uundwaji wa Serikali za Umoja wa Kitaifa? Serikali hizo ni kwa manufaa ya viongozi au wananchi? Ni yapi wananchi wa Zimbabwe, Kenya, Zanzibar n.k wanaweza kufurahia kwamba yameletwa na Serikali za Umoja wa Kitaifa?

Je ni mfumo ambao Tanganyika tunaweza kuufuata hivyo CHADEMA waanzishe vurugu CCM wakatae kuachia madaraka. Wengine wachochee udini na ukabila ili tuvurugane mwishoni tuunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa???

Nawasilisha!!:sing:

tujifunze kwanza tija ya serikali ya umoja wa kitaifa kutoka zanzibar, tuwape miaka kumi ili tujue kama inafaa au la
 
Hata wewe Mzambia?

I deliberately left questions unanswered expecting that a discussion will ensue and at the end conclusions be made. I had expected that we will be able to highlight the pros and cons of GNU's. Still we can do that and I can defend the presentation as I do that it is not crap!

Btw did you mean C-R-A-P as in Carefully Researched and Presented?

Then thank you very much.
 
Back
Top Bottom