Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Salaam wakuu,
Serikali za Mitaa zinaundwa na sheria No.7 ya mwaka 1982.Hii ni baada ya Sheria ya Madaraka Mikoani ya mwaka 1972 kushindwa.
Katiba ya JMT ya mwaka 1977,Sura ya 8 Ibara za 145 na 146 inaainisha muundo na majukumu ya Serikali za Mitaa.
Nimeshangazwa sana na maagizo ya Rais wa Tanzania Mh.Magufuli kuagiza Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es salaam kukaa kikao ili kujadili matumizi ya TSh.5.8 bilioni zilizolipwa na kampuni ya UDART.
Madiwani wana vikao vyao na taratibu zao za kuitisha vikao.Wana Mstahiki Meya na Wenyeviti wa Halmashauri.Hawahitaji maagizo ya Mh. Rais ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku.Kuwaagiza kufanya kikao ni kuwaingilia!