Serikali za mitaa na maendeleo ya jamii

JMWAKA

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
727
633
Na Mwananchi wa kawaida

suala la kwanza Kabisa wenyeviti wa mitaa kisheria wanapaswa kufanya Mikutano ya mitaa kila baada ya miez miwili ili wananchi watoe Maoni yao kuboresha v Maendeleo ya mitaa

Pia Kama serikali ya magufuli imetangaza mapato na matumiz kwanini serikal za mitaa isibandike mapato na matumiz ya mitaa sababu Kama ni suala la uuzwaji na ununuaji WA viwanja na majengo kuna 10 percent ianayobak serikal ya mtaa hilo ni pato ambalo linahitaji mipangilio ya Maendeleo ya mtaa na baadae matumiz yake kuwekwa waziwazi Kabisa

Mambo ya kuboreshwa zaidi ni kufanyika ugatuzi wa madaraka kwamaana Viongoz wa serikali za mitaa kupatiwa nguvu zaidi kisheria za kufanya maamuzi yenye tija kwa eneo husika lakini maamuzi hayo yawe na limitation zake ambazo ni Mikutano mikuu ya mtaa

Suala la muhimu Hawa watendaji wa mitaa wanaoajiriwa na serikali itakuwa vizuri wakawa ni wakazi wa kidumu wa eneo husika kuliko mtendaji WA mtaa A anaishi Mtaa C litasaidia utekelezaji mzuri wa Majukumu

Kama Sheria inaruhusu mitaa kujitungia Sheria ndogo ndogo sasa wanashindwaje wenyeviti kutunga Sheria ndogo ndogo kudhibiti masuala ya usafi, ulinzi kushirikiana na polisi na polisi jamii pamoja na masuala ya Afya eneo husika

pia Haya mapato yanayokusanywa kutokea s/mitaa mengine yabaki ili kutekeleza miradi ya ndani ya mtaa inayoweza kusimamiwa vizur na wenyeviti pamoja na wajumbe wake Kama barabara za mitaa uwekaji wa dustbin kila kona ya mtaa na usafi wa mitaa kiujumla na Maendeleo ya mitaa husika na kuwawezesha vijana kujiajiri ndani na nje ya mtaa husika hapo tatizo la Ajira litaanza kupotea kidogo na kuisha Kabisa
BY
Comred JOSEPH MWAKATOBE

Hoja au Maoni Karibu kujadili
 
Back
Top Bottom