Serikali yawajibu UKAWA kuhusu safari za Rais

...taarifa ya kijinga sana hii....na inadhihirisha jinsi wizara yenyewe inavyofanya kazi kimagumashi.....Nawataka wizara hii wanijibu swali moja tu....alafu mengine yote yatakuwa yamejibiwa.....wizara iwaambie watanzania...je kila safari moja ya JK inagharimu kiasi gani???....namaanisha kila safari katika mabara yoote aliyosafiri kwa miaka 10...watuambie gharama za safari.....alafu sisi tutadadavua jumla ya gharama....maana safari zake tuna takwimu zake humu.....wizara waache magumashi.....watupe gharama za kila safari(maana wanajua).....na kama wanawajali kweli watanzania basi pia waseme faida (kimapato)kwa nchi kutokana na safari hizi...

....Nilitegemea wizara wangekuja na mchanganuo wa gharama za kila safari za JK vs faida zake (mapato kwa nchi)....vinginevyo hadithi zote ni blah blah tu...tumewazoea....

Ndugu yangu Nderingosha,hawawezi na hawathubutu kuweka facts hizo humu.Usisahau kwa halisi ilivyo nchini,hakuna wizara wala idara iliyo salama kimaadili.
 
hahahaha dogoooooo siandiki kukufurahisha ww.... na sijui kipimo chako cha upeo ni kipi?

Taarifa ya serikali imefafanua kiasi cha kutosha lakini ama kwa uchanga wa akili yako au ushabiki ulionao umeshindwa kuielewa taarifa hiyo. Kipimo changu cha upeo ni jinsi unavyoweza/unavyoshindwa kuelewa hoja ambayo iko very stright forward mbele yako.
 
Kuna wakati ilitolewa taarifa kuwa kuna wajanja wamekwapua pesa ya safari za rais.
 
Umaskini wa akili ni mbaya zaidi ya umaskini mwingine wowote.Kuna baadhi ya watu ambao hata wazazi/waalimu wao walinyanyua mikono kwa kuuchoka ununda wao!
Umetoka mchanganuo unaoeleweka na kwa lugha ya kiswahili...lakini bado anatokea punguani na kumwita Rais Vasco Da gama.Huu ni ukosefu wa adabu.
Wapo wanaofikiri kwamba anapojisikia Rais kusafiri basi anaamua tu kwa ajili ya kwenda kutazama magorofa ya Ulaya/Marekani.
Nchi yetu ipo katika jumuiya ya kimataifa.Yapo masuala mengine yanayohusu nchi yetu au Ukanda fulani,anatakiwa awepo Rais mwenyewe kama Rais na si vinginevyo.Sas inapotokea kasafiri basi inakuwa nongwa na uzushi usio wa maana.
Upinzani katika Afrika ili uitwe upinzani panatakiwa elimu ya miaka si chini ya kumi japo kidogo watu wataelewa.Wengi wetu hatuelewi nini maana ya upinzani wa kisiasa.
katika nchi yetu upinzani ni kupinga kila kitu,kuongeza chumvi,unafiki na porojo za kilevi.
Mfano: Wapo watu wazima na akili yao inayofikiria mwisho wa pua zao walizusha na wanaendelea kuaminisha watu kwamba Rais wa kwanza wa Tanzania,Julius Nyerere alikuwa anayo TV yake pale Msasani na alikuwa akiangalia kwa siri matukio duniani halafu huja hadharani na "kuwadanganya" watanzania kwamba Marekani au Urusi kuna jambo fulani baina yao.ilimradi tu aonekane ana akili!!
Lakini na wale wanaoambiwa porojo hizo wengi wao maskini hawatafakari! Wanalipokea na kulieneza lilivyo.Hii ni hatari sana.
Hatokei mmoja akahoji: Hivi wakati wa Mwalimu palikuwa na kituo chochote cha kurushia matangazo (ukiacha Zanzibar)?Jibu ni hakuna!Na ili matangazo ya TV yapatikane mahali fulani si panahitaji mitambo ya kurushia matangazo? na je, wakati wa utawala ule Teknolojia ilikuwa kwa kiwango gani?na je,Mwalimu kama Rais hakuwa na vyanzo vingine vya habari hata nje ya Tanzania mpaka ifikie kufanya mambo wanayoyasema baadhi ya watu?
Jibu ni kwamba Rais kama mkuu wa nchi ana vyanzo vingi vya kupata habari (Information sources).
Kwa akili ya baadhi ya watu hudhani kwamba rais anajiendea tu kwa utashi wake anapoamua basi!
Kwa hivyo kama ilivyo kawaida wapika majungu wameileta hesabu yao ya safari za Rais hadharani(wakati bajeti zao hatuzijui) na serikali imetoa mchanganuo wake.
Nafikiri wakinaswa hao wapotoshaji na sheria ya cyber crime na wakahukumiwa itapunguza watu kuzusha ujinga kama huu.
Ujerumani ilianzisha vita kuu vya pili vya dunia kwa ujinga kama huu.Maneno ya uzushi,propaganda,uongo,fitina,uchochezi wa kugawa watu na mwishoni mamilioni ya watu waliteketea.Wanajuta kumjua Adolf Hitler.
Tubadilike jamani!

Shame on you!!! Fikiria kabla ya kuandika na kuanza kutukanatukana!!!! Yaani kweli huoni hata aibu kuonyesha umburura wa kiasi cha hali ya juu kama chako???? Tumia hata kidogo basi akili aliyokuma Mwenyezi Mungu!!!!

Historia yako ya maendeleo na choko choko za vita ya pili ya dunia ziko kushoto kabisaaaa!!!! Ndio maaana tunasema kipaumbele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu!!!!!

Nitajia nchi hata moja duniani ambayo imeendelea kwa misaada ya nchi nyingine???? Au Rais wake kuwa mzururaji duniani????

Hivi huoni hata aibu kuandika ----- huuu ulioweka hapa kwenye Home of Great Thinkers???? Kipindi cha miaka 20 ya Rais mstaafu J. K. Nyerere, nchi ilipata ustawi wa maendeleo wa hali ya juu, viwanda vilishamiri kila mkoa, kazi na uwajibikaji ndio uliokuwa mfumo wa serikali.

Katika kipindi hiki cha miaka 20, safari za Baba wa Taifa hazifiki hata nusu ya safari za Rais anayemaliza muda wake J.M. Kikwete, kwa kipindi cha miaka 10 hakuna hata kiwanda kimoja kilichojengwa na Serikali, hachilia mbali ujenzi wa kachuo kamoja cha Vacational Training Centre Njombe.....
 
Hii nchi hii wizara nzima inajibu kipuuzi namna hii? dah laana iko juu ya Tz


Huko wananazo kweli ................ kama wameamua kujibu basi waseme ni safari ngapi amefanya na siku ngapi katumia na gharama kiasi gani kwa ujumla. Hii ya kupiga juu juu ni kulikuza hili jambo. Bora wangekauka tu kama kawaida yao!!
 
Kiongozi, ndo I.Q ya viongozi wa C.C.M, wewe unategemea nini kama mpeperusha bendera wao wenyewe anasema Sadam Hussein anatokea Kuwait????, Ndo maana vipaumbele vya UKAWA cha kwanza hadi cha tatu ni Elimu, Elimu, Elimu.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi anaitwa nani vile?
 
Hao wanao sema eti raisi anatumia pesa nyingi katika raisi ziara zake' mbpna hamsemi pia kutokana na ziara zake kuingiza sh.nhgapi nchini!!
Alafu bajeti ya safari za wakuu wa nchi ziliizinishwa bungeni pale dodoma, iweje leo aseme (Mbatia) kuwa raisi anatumia pesa nyingi katika safari zake kwa kipindi cha miaka10 ya utawala wake!!! "RECKLESS STATEMENT"
 
Hiyo wizara isiwaone watanzania wa leo ni walewale wa mwaka 47,mbo hamkukanusha kuhusu Richmond mmekaa kimya mpaka leo,tafadhalini litoleeni ufafanuzi na hili la Richmond ni nani mwenyenayo?tafuteni igizo jingine hatudanganyiki na mmepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom